YESU NI JIBU

Jumatatu, 19 Mei 2014

FUATILIA KWA MAKINI JINSI YA KUMLEA MTOTO WAKO USIJE UKAJILAUMU SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO




MAKUNDI 4 MUHIMU YA MABADILIKO NA MAKUZI YA MTOTO!


Kwa mujibu watafiti wa saikolojia ya watoto kuna makundi manne ya muundo wa kimakuzi na kimaendeleo ya kiakili kwa mtoto

I. MWAKA 0 – 5
1. Mtoto kwenye kundi hili huwa na swali moja tu – NINI? What is this.
2. Hiki ni kipindi cha mtoto ku “register” vitu vya aina mbalimbali. Kumbuka kwamba mtoto ndiyo kwanza ameingia katika dunia hii na kila kitu anachokiona ni kigeni ndiyo maana katika umri huu mtoto anaswali moja tu Hii ni nini? What is this?

3. Wazazi wengina hufanya kosa kwa kuona kero kumjibu mtoto mara kwa mara anapokuja kuuliza hii ni nini. Wakati mwingine mtoto anaweza kuja kukuuliza swali hilo hilo kwa kitu kile kile mzazi anakasirika maana anaona mbona tayari nilimjibu ananisumbua tena kwa hiyo anamjibu vibaya au hamjibu kabisa.

4. Hiki ni kipindi ambacho mzazi anatakiwa atumie mtindo wa KUTAWALA katika kumlea mtoto wake. Katika kipindi hiki mzazi anatakia kutumia nguvu ya kutawala kumtengeneza (“shape”) mtoto katika njia njema.

5. Mtoto katika kipindi hiki asikuendeshe na kukutawala badala ya wewe kumtawala. Mfano mtoto analilia kuchezea simu na ukimpa anaibonda bonda chini au kuitupia kwenye maji na ukimkataza anaanza kulia basi ili anyamaze inabidi tu umpe hicho anacholilia hata kama ni cha thamani. Kwa kufanya hivyo unalipeleka (forward) tatizo mbele kwani atakapoingia kwenye kipindi cha pili utapata shida sana ya kuliondoa hilo tatizo na litaendelea kukua.
Kuna siku atalilia umtungulie mwezi angani sasa sijui hapo utaazima ngazi wapi umpe kila anacho kililia.

II. MIAKA 6 – 9
1. Mtoto katika kundi hili swali lake kubwa huwa ni “HOW” INAKUWAJE.

2. Hiki ndio kipindi ambacho mtoto hunyonya nguvu ya mahusiano kutoka kwa mzazi. Katika kipindi kilichopita yaani miaka 0 -5 hata kama hakutakuwa na mahusiano ya kina sana haijalishi sana kwa mtoto kwani ile misuri yake ya mahusiano huwa imekomaa kuanzia kipindi hiki.

3. Hiki ndio kipindi muhimu sana kwa wazazi kuhakikisha kwamba wanaweka ratiba kabisa ya kujenga mahusiano na watoto wao.

4. Hapa ndipo msingi wa ghorofa la mahusiano unapochimbiwa. Mzazi akipuuzia kufanya kazi ya kuchimba msingi wa mahusiano hapa kwa hakika itamgharimu kule mbele ya safari. Utajaribu kujenga ghorofa kule mbele ya safari lakini litakuwa linadondoka kwasababu utakua unajenga ghorofa juu ya ardhi ya mahusiano isiyo na msingi.

5. Usipojenga mahusiano mazuri na yakaribu katika kipindi hiki, kuna baadhi ya tabia mbaya zitajengeka kwa watoto na kuna wakati utakuwa unataka kuziondoa haitawezekana ndiyo wazazi wengine wanachanganyikiwa kutokana na mambo yanayofanywa na watoto na kwa wakati huo inakuwa haiwezekani tena kuwabadilisha.

6. Kutokana na mfumo wa kimaisha, wazazi wengi wapo na mihangaiko ya (BIZE) kutafuta pesa hawana muda na watoto wao kwaajili ya kuwambukiza joto la maadili mema. Mzazi hana muda na watoto anakwenda kazini au biashara asubuhi na anarudi usiku na hata akirudi anakuwa amechoka anapitiliza kulala au anaendelea na kazi zake hata akiwa nyumbani. Anapoteza jambo la msingi sana ambalo litakuja kumgharimu mbele ya safari na kwa bahati mbaya wengi huwa hawana uwezo wa kulipa hizo gharama kwani sio za pesa wala mali ni gharama za mahusiano.

7. Wazazi wengi wanaliwa na “PEPO” la maendeleo. Baadhi ya wazazi wanawapeleka shule za kulala “boarding” watoto wao wadogo walio kwenye kundi hili. Wanafikiri ni maendeleo wanajionea fahari mtoto anarudi anaongea kingereza. Mimi nakwambia mtoto atarudi anaongea kingereza lakini atarudi pia na roho za ushoga na usagaji na madudu mengine kwani utafiti unaonyesa watoto wengi waliwekwa mbali na wazazi wao na kuishi kwenye mazingira kama hayo hupata nafasi kubwa ya kujifunza mambo kama hayo ambayo huwachukua muda mrefu sana kuja kuwa toka na wengine huendelea nayo mpaka wanakuwa watu wazima bila hata mzazi kuweza kugundua kwani hufanya siri sana. Mimi binafsi nimefanya ushauri “counseling” ya vijana wengi mashoga, wasagaji na wengi wao husema walijifunzia shule za bording wakiwa katika umri huu.

8. Baadhi ya wafanya kazi wa ndani pia huchangia kuwafundisha tabia mbaya watoto wadogo katika kundi hili. Kama mzazi hatakuwa na mahusiano ya karibu na mtoto hataweza kugundua kabisa kinachoendelea nyuma ya pazia katika maisha ya mtoto.

III. MIAKA 10 – 14
1. Mtoto katika kundi hili swali lake kubwa huwa ni WHY? KWANINI?

2. Hiki ni kipindi ambacho misuli ya kichwa cha mtoto imeanza kukomaa na kuweza kufikiri kwa kina zaidi.

3. Hiki ni kipindi ambacho mzazi anahitajika kuwa na sababu mkononi.

4. Unapomwambia mtoto usifanye 1, 2, 3 kwa upande wa pili mzazi anatakiwa awe za sababu kwanini anamwambia mtoto asifanye hivi na hivi. Au ukimwambia mtoto nataka ufanye hivi na hivi hakikisha unasababu mkononi kwanini unamtaka mtoto afanye hivyo.

5. Ukifanya hivyo mtoto atafanya jambo kwa moyo ana kiwango cha kukuheshimu na kukupenda kitaongezeka.

6. Ni vema mzazi ukajua kwamba hiki ni kipindi ambacho mtoto huwa makini sana “very sensitive” kuliko kipindi kingine na hujisikia kufanya jambo kwa kujiamini akiwa anajua sababu zake.

7. Hiki sio kipindi cha kutumia nguvu kwamba nimesema kama mzazi fanya hivi na sitaki maswali maswali hiyo itakuwa ni kubomoa badala ya kujenga hasa kwa siku za usoni katika maisha ya mtoto.

MIAKA 15 – 17
1. Hiki huwa ni kipindi kigumu sana kwa wazazi walio wengi sana. Kipindi hiki huwa kigumu zaidi kwa mzazi hasa kama hatua hizo hapo juu hukufanya vizuri.

2. Baadhi ya wazazi hupuuzia hatua hizo hapo juu hatua ya 1 hatua 2 na hatua 3. Wanapofika hatua ya 4 wanagundua kwamba kunakitu hawakufanya wakati mtoto anakua na sasa ndiyo wanakurupuka kutaka kumrekebisha mtoto na kumfundisha maadili mema tayari umechelewa. Ndio maana nilisema usipozingatia zile hatua za awali ukifika hatua ya 4 utalipa gharama.

3. Mtoto katika kundi hili swali lake kubwa huwa WHAT IS THIS, I WANT TO TRY. Hujiuliza HII NI NINI, NATAKA KUJARIBU.

4. Hiki ndio kipindi ambacho chochote ukimwambia mtoto usifanye hivi na hivi katika kipindi hiki, ndio kama kumtuma kufanya hicho unachomkataza.

5. Mzazi ukikurupuka na kuanza kumfundisha mtoto katika kundi hili kwamba tendo la ndoa sio zuri kwa watoto subiri mpaka utakapokuwa mtu mzima. Basi ujue hapo ndio kama umemchochea kujiuliza zaidi hivi hili tendo la ndoa ni nini? Nataka kujaribu.

6. Hiki ndio kipindi ambacho watoto hutaka kujaribu kila kitu hata vile ambavyo wameambiwa au wamekuwa wakisikia kuwa ni hatari.

7. Hapo ndipo watoto hutaka kujaribu vitu kama sigara, bangi, tendo la ndoa, madawa ya kulevya n.k

NAMALIZIA KWA KUSEMA KILA MZAZI ACHUKUE JUKUMU LAKE KIKAMILIFU KULEA MTOTO SIO KAZI YA “by theway”
 Ndugu msomaji ni jukumu lako kuamua kufanyia kazi haya yote ambayo umeletewa na mwalimu na mchungaji Peter Mitimingi mkurugenzi wa VHM sasa usipofanyia kazi nani wa kumlaumu mwanao akiharibikiwa,bila shaka utajilaumu mwenyewe na utabeba lawama hizo mwenyewe.
Bottom of Form

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni