Falsafa ya
umikilishaji kwa mujibu wa Biblia
Katika toleo lililopita tulisoma kuhusu baadhi ya mambo
muhimu katika sera ya MVIMAUTA. Leo nimeona ni muhimu nikushirikishe mambo
yaliyojiri siku ya Uzinduzi kwa kukupa sehemu ya Risala niliyoisoma mbele za
Mgeni wa Heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kisha mbeleni niletee sehemu ya hotuba
yake ya Uzinduzi. Leo tuanze na Risala ya Uzinduzi:
Risala ya
Uzinduzi wa MVIMAUTA
Falsafa ya
umikilishaji kwa mujibu wa Biblia
Katika toleo lililopita tulisoma kuhusu baadhi ya mambo
muhimu katika sera ya MVIMAUTA. Leo nimeona ni muhimu nikushirikishe mambo
yaliyojiri siku ya Uzinduzi kwa kukupa sehemu ya Risala niliyoisoma mbele za
Mgeni wa Heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kisha mbeleni niletee sehemu ya hotuba
yake ya Uzinduzi. Leo tuanze na Risala ya Uzinduzi:
Risala ya
Uzinduzi wa MVIMAUTA
Taarifa fupi ya Mpango
Mpakati wa kwanza
“Mheshimiwa Rais, huu ni mwaka wa
tatu, tangu ulipotutembelea mwaka 2010 na kutuzindulia Mpango Mkakati wa miaka
10 kwa jina maarufu la MAADILI KWA KIZAZI KIPYA. Mpango huo ulizinduliwa ukiwa
na mikakati mikuu 3 ambayo ni
1. Urejesho wa Maadili katika jamii
2. Unoaji wa vipaji vya uongozi kwa kizazi
kipya
3. Kumilikisha uchumi endelevu
Jinsi mikakati hii
ilivyotekelezwa:
v Urejesho wa Maadili
Mkakati wa Urejesho wa maadili
ulifanyika chini ya kampeni maalum iliyovuma kwa jina la OPERESHENI TAKASIKA
ambapo idadi ya watu zaidi ya 72,000 elfu walielimishwa kurejea kwenye maadili
ya kiimani.
Kwa upande wa vijana, tuliweza
kuwafikia zaidi ya 6,000 kwa kupitia semina na makongamano mbali mbali hapa
jijini DSM
v Unoaji wa vipaji vya uongozi
Mkakati wa kunoa vipaji vya
uongozi, tulifanya utafiti ni kwa jinsi gani tunaweza kubaini vipaji wa uongozi
miongoni mwa vijana na kuvikuza kwenye misingi ya maadili. Njia pekee
tuliyoibani ni kuanzisha Chuo Kikuu cha uongozi wa kimaadili kwa jina la Moral
Leadership University. Mpaka hivi sasa mchakato wake umefikia kuundwa kwa
Baraza la Chuo, na Utawala wake ambao DVC wake ni Profesa Immanuel Bavu.
Tulikwisha kuwasilisha maombi yetu
kwenye Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) pamoja na kwamba tulikamilisha taratibu zote za
kupata usajili ikiw ani pamoja na kukodi majengo ya muda ili tuanze kozi za
muda mfupi, hatukufanikiwa na tukashauriwa kutafuta eneo jingine tofauti nna
mahali pa awali na mpaka hivi sasa tupo katika mchakato huu kutaka kujenga chuo
hiki kuanzia katika viwanja hivi!
Baada ya kuona tunazidi kuchelewa,
tumeamua kuanza mchakato wa kuanzisha taasisi ya kukuza vipaji kwa jina la
TANZANIA INSTITUTE OF TALENTS (TIC), ambao Profesa Bavu anaendelea nao mpaka
hivi sasa.
Mheshimiwa Rais, tuna imani kwamba
ikiwa tutaweza kupata usajili wa taasisi hizi mbili, tutakuwa na uwezo wa
kutekeleza mkakati wa kunoa vipaji vya uongozi wa kizazi kipya kama maono yetu
ya awali yanavyoelezea.
v Utekelezaji wa Mkakati wa kumilikisha uchumi endelevu
Mkakati huu tuliutekeleza kwa
kufanya mambo muhimuu yafuatayo:
1. Mafunzo
ya uchumi uliojengwa kwenye maadili
Tuliendesha
semina na makongamano na kuhamasisha elimu ya kubuni miradi ya kujipatia kipato
cha uhakika badala ya kutegemea ajira ambazo fursa yake ni finyu
2. Utafiti wa miradi
yenye matokeo ya haraka
Kufanya
utafiti juu ya miradi ambayo inastahili kuanzishwa na kuleta matokeo makubwa
kwa muda mfupi. Mradi ambao tulibaini unaweza kutupa matokeo makubwa kwa haraka
ni kilimo cha umwagiiliaji.
Tumeamua
kuunga mkono juhudi za serikali yako za mikakati ya kuleta MATOKEO MAKUBWA
SASA:
ü Chanzo cha matokeo makubwa ni
“Maono makubwa”
ü Maono makubwa huzaa mipango
mikubwa ambayo huleta matokeo makubwa
ü Lakini siri kuu iko kwenye neno
“SASA”! Huu ni usemi wa kiimani wa uumbaji wake Mungu. Sisi tunaona hii ni
kauli ambayo Mungu aliitumia kuumba vitu vikatokea mara moja pasipo kusubiri
mchakato
Lakini pia
tulibaini changamoto zilizopo katika mradi huu ambazo ni upatikanaji wa ardhi
inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, na miundombinu ya umwagiliaji ambayo
gharama zake ni kubwa.
Lakini kwa kuwa tulikwisha
kupania kuanza mradi huo tumejitahidi kununua ardhi kiasi cha ekari 430 za
kilimo cha mpunga Ifakara, ekari 300 za kilimo cha ufuta Kibaha na ekari 100 za
kilimo cha vitunguu Mang’ola juu Arusha.
Kimsingi, haya tumeamua
kuyafanya yawe mashamba darasa kwa ajili ya mafunzo ya kilimo wakati jihudi
zinaendelea za kupata hekta 6,000 huko huko Morogoro vijiji vya Kingwa na
Kisaki.
Lakini lengo
letu kuhusu upatikanaji wa ardhi tunatamani kupata ekari zisizopungua ekari
500,000 ambazo watamilikishwa vijana kwa ajili ya miradi ya kilimo na matumizi
mengine ya ardhi
3 Wazo
la kuunda mtandao wa vikundi vya maadili na uchumi Tanzania (MVIMAUTA)
Mheshimiwa
Rais, suala la umilikishaji uchumi ni zito na si rahisi kummilikisha kila mtu
mmoja mmoja katika jamii. Katika kutafuta mbinu za kumilikisha uchumi tumebuni
mkakati wa kuanzisha rasmi mtandao wa vikundi vya maadili na uchumi ambao
kimaadili utasimamiwa na WAPO MISSION INTERNATIONAL, lakini kiuchumi usimamiwe
na BISHOP GAMANYWA FOUNDATION na utunzaji wa fedha usimamiwe na OMEGA SACCOS.
Wakati huo huo WMI imeteua Kampuni maalum ya BSHG Consultants Ltd (kwa
kushirikiana na wataalamu wa serikali) isimamie mafunzo na uendeshaji wa miradi
ya kilimo kwa ajili ya vikundi vya mtando huu mpya.
Sera ya Mtandao
wa Vikundi vya Maadili
na Uchumi
Tanzania (MVIMAUTA)
v Maono, dhima na lengo kuu
Maono ya Mtandao wa Vikundi vya
Maadili na Uchumi Tanzania (MVIMAUTA) ni;
“Kufikia mwaka 2028, vijana wa Tanzania wawe wanamiliki uchumi
endelevu ambao msingi wake ni ardhi
inayomilikiwa na watanzania wenyewe”.
Dhima kuu ni; “Kuhamasisha na
kuwawezesha vijana kumiliki uchumi kupitia vyanzo vikuu ambavyo ni; ardhi,
madini, mifugo, maji, na kilimo”.
Lengo kuu ni; “Kumkwamua kijana
kutoka katika hali ya umasikini hadi awe na makazi yake mwenyewe, ardhi kwa
ajili ya kilimo, na shughuli halali za kumuingizia kipato”.
Walengwa wakuu wakiwa ni makundi
ya: Vijana wanaohitimu katika vyuo vya kati na vyuo vikuu na wanashindwa
kupata ajira; Vijana waishio mijini kwa kufanya biashara ndogo ndogo zisizoweza kukidhi
mahitaji yao ; Vijana waishio vijijini wenye kutegemea kilimo cha jembe la mkono peke
yake; Vijana wajasiriamali walioanzisha miradi midogo ya biashara; Wanandoa
na wazazi/walezi kama wadau muhimu katika urithishaji
v Umuhimu na upekee wa MVIMAUTA
1.
Muunganiko wa
maadili na uchumi.
Kwa karne nyingi kanisa la leo
limetenganisha ”Maadili na uchumi” kama vitu visivyo na uhusiano. Hali hii
imesababisha udhaifu badala ya ufanisi. Kulingana na tafiti zilizokwisha
kufanyika huko nyumba, taarifa zake zilibainisha kwamba, ”uchumi bila maadili” huzalisha ufisadi
katika jamii. Na kwa jamii ya kitanzania hiki ndicho kinachosababisha
malalamiko na lawama dhidi ya wanaodaiwa kuitwa ”mafisadi”! Pili “Maadili bila uchumi ni kudumisha ufukara katika jamii»
2. Fursa ya kukuzaji vipaji vya uongozi
UVIMAUTA unakuja
na fursa pekee ya kukuza vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana watakaojiunga
na mtandao huu. Kumbuka kwamba, kila kikundi cha watu ishirini kitakuwa na
kiongozi wake. Na kila kikundi kizima
kinapoundwa kitapata mafunzo ya uchumi na uongozi.
Katika mafunzo ya
uongozi kila mwanakikundi anatafsiriwa kuwa ni ”kiongozi mtarajiwa” wa kikundi
kipya atakachokiunda yeye mwenyewe. Hivyo hivyo zoezi linaendelea la ”vikundi
kuzaa vikundi” ambapo mafunzo ya uongozi huendelea na fursa mpya za uongozi
kupatikana kwa kuundwa vikundi vipya.
3. Fursa ya kukuza mitaji kupitia mtandao
Kikwazo kikubwa
ambacho kinadaiwa kuendeleza umaskini wa kipato katika jamii, ni ukosefu wa
mitaji. Kila mwenye wazo la kufanya mradi wa uzalishaji anajikuta anakabiliwa
na changamoto ya ukosefu wa mtaji. Wakati huo huo njia pekee iliyopo ya kupata
mtaji ni mikopo kuotka katika taasisi za fedha. Masharti ya kukopesha ni
mkopaji kuwa na dhamana ya nyumba au mali yenye thamani inayozidi kiwango cha mkopo
anaoutaka. Wengi hawana dhamana na hivyo kujikuta hawakopesheki.
MVUMAUTA unakuja
na jawabu la miaka mingi la ukosefu wa mitaji. Mfumo wa kuunda vikundi
unashughulikia changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa sababu, watu ishirini
wanaweza wenyewe kuchangiana mitaji kwa zamu na kila mmoja wao kupata mtaji
mkubwa wa mradi anaotaka kuufanya, na bila masharti ya kutoa dhamana.
Aidha, kikundi
kinapojiunga katika mtandao huu, tayari kinakuwa kimeingia katika jamuiya
ambayo vitakuwepo vikundi vingine ambavyo vimeanzishwa kwa madhumuni ya
uwezeshaji wa vikundi visivyo na mitaji; ili mradi vitaingia ubia ambao
utahusisha kugawana faida baada ya mauzo.
Huu ni uwezo wa
ndani ya vikundi wa mtandao wenyewe. Isitoshe, kwa kupitia mtandao huu, kuna
fursa ya kuziendea taasisi za fedha na kuziomba mikopo kwa ajili ya miradi ya
mtandao na dhamana ikawa ni mtandao wenyewe kwa taratibu ambazo zi lazima
kuzielezea kwa hivi sasa.
Hapa fursa ni Mtandao wenyewe kuwa dhamana ya mikopo
ya vikundi badala ya wana vikundi kusumbuka kuweka dhamana ya mali zao binafsi
4.
Fursa ya kuibua na kuendeleza vipaji
Kutokana na ripoti
ya maoni ya vijana wasomi wa vyuo vikuu ambayo ndiyo imechangia kuundwa kwa
mtandao huu; imebainika kwamba elimu inayotolewa na sekta yetu ya elimu, haina
mikakati ya kuibua na kukuza vipaji, bali imejaa nadharia tegemezi. Kwa mantki
hii mpaka sasa kuna upungufu wa fursa za kubaini vipaji mbali mbali na
kuviendeleza kwa kuviwezesha kimafunzo na mazoezi kwa viwango vya kimataifa
MVIMAUTA utatoa
fursa kupitia vikundi vyake kutoa mafunzo na mazoezi ambayo gharama zake
zitatokana na miradi maalum kwa madhumuni hayo.
Isitoshe, kuna taasisi ya Bishop Gamanywa Foundation (BGF) imeanzishwa kwa
maono ya kufadhili mafunzo na mazoezi ya ukuzaji vipaji. MVIMAUTA untanufakika
na taasisi hii katika eneo hili lililotelekezwa!
Itaendelea
toleo lijalo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni