YESU NI JIBU

Jumamosi, 17 Mei 2014

SHIRIKIANA NA MTUMISHI P.K.E WA HOUSE OF PRAYER CENTER

Ni wakati wa kufunguliwa kutokana na nguvu za giza na mateso ya pepo wachafu na hii inatokana na mwamini kusimama na kujifunza neno la MUNGU na kuhuhuria kwenye mafunndisho ya neno la MUNGU na maombi na maombezi.
Hii imedhihirika katika nyumba ya maombi (H.P.C) iliyoko Tabata Sanene katika eneo la Ugombolwa,huduma hiyo inaongozwa na mtume Patric Kayimbi ambaye kwa sasa amefungua matawi ya huduma hiyo katika mikoa mbalimbali
Akizungumza na blog hii mtumishi wa MUNGU PKE alisema kuwa kwa sasa anasimamia kazi ya hiyo ya MUNGU kwa lengo la kuleta nafsi kwa YESU.
Hata hivyo apostle PKE amewataka waumini kujitokeza kushiriki maombe  na maombezi kwa lengo la kunguliwa na sambamba na kuliombea taifa amanio kwani bila amani hakuna kitakachoweza kuendelea, hata kushiriki katika ibada itakuwa ni vigumu sana hivyo ni jukumu la kila mwamini bila kujali dini yake kusimama na kuombea Taifa la TANZANIA amani.
Hata hivyo apostle PKE amekuwa na jitihada za kuwakaribisha wageni mbalimbali kuja kuhubiri na kufundisha neno la MUNGU kwa waumini wa huduma hivyo na wengi wamefunguliwa na matatizo mbalimbali.






Hakuna maoni :

Chapisha Maoni