Muuguzi Namubiru aliambia mahakama
hakuwa na nia ya kumuambukiza mtoto huyo HIV
Nchini Uganda mahakama imempata na
hatia muuguzi mwenye HIV, aliyeshitakiwa kwa kumdunga mtoto mchanga sindano,
ambayo awali ilimchoma yeye mwenyewe.
Muunguzi huyo, Rosemary Namubiru,
mwenye umri wa miaka 64, mwathiriwa wa virusi vya HIV, amefungwa miaka mitatu
jela, kwa kile hakimu amekiita, 'uzembe wa weledi'.
Taarifa
zinazohusiana
Hukumu hio imetolewa wiki moja baada
ya bunge la Uganda kupitisha muswada, unaomtia hatiani mtu yeyote ambaye kusudi
anamuambukiza mtu mwengine virusi vya ukimwi.
Mtoto huyo hata hivyo hakuambukizwa
virusi vya HIV na wanaharakati wamekosoa mahakama kwa kumfunga jela mwanamke
huyo.
Rais anasubiriwa kuidhinisha au
kutupilia mbali mswada wa adhabu kwa wanaombukiza wengine HIV kusudi
Babake mtoto huyo hata hivyo
alielezea kufurahishwa na uamuzi wa mahakama.
Baba huyo, Daniel Mushabe, amesema
kuwa anatumai kesi hiyo itampa motisha Rais Museveni kuidhinisha mswada
uliopitishwa na wabunge wa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaowaambukiza
wengine HIV kusudi.
Adhabu ya kosa hilo ni faini ya dola
1,900 au miaka kumi jela.
Sheria hiyo ikiwa itapitishwa
itawaadhibu wanaotenda uhalifu huo kwa maksudi.
Wananchi bila shaka walionyesha kuudhiwa
na kitendo cha muuguzi huyo ingawa wanaharakati wamemtetea mama muuguzi.
Hakimu aliyetoa hukumu alisema kuwa
Namubiru alikosa kuonekana kama aiyesikitishwa na kosa lake.
Namubiru, muuguzi mwenye uzoefu wa
kazi wa miaka 30, alisisitiza kwamba hana hatia na kuwa mtoto huyo
hakuambukizwa HIV.
Namubiru aliamua kumdunga sindano
mtoto huyo kutafuta mshipa lakini kapata ugumu na hivyo kujidunga mwenye kwa
bahati mbaya lakini amesisitiza kuwa hakuwa na nia yoyote ya kumuambukiza mtoto
huyo virusi vya HIV.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni