YESU NI JIBU

Jumatatu, 26 Mei 2014

FURAHA TELE NDANI YA KANISA TAG MABIBO SAHARA KANISA LA NGUVU NA NEEMA.



 Shangwe, nderemo  na vivijo yalijitokezaa katika kanisa la TAG Mabibo Sahara mara baada wa kija wa Askofu masawe kutangaza uchumba katiaka kanisa hilo miss Tumaini.
Akizungumza katika shuguli hiyo ya ya kutangaza uchumba mchungajib aliyealikwa kwa ajili ya shughuli hiyo rasmi ,chungaji wa kanisa la TAG magomeni mchungaji Kanemba alisema kuwa hiyo ni moja ya hatua kubwa ya kufanya maamuzi ya kuwa na mtu mwingine katika maisha ya kila mtu.
Aidha alisema kuwa ni vyema vijana wakae chini ya uongozi wa MUNGU ili kila jambo lenye baraka wanalowaza kufanya liwe na uwepo wa  MUNGU.
Akifundisha somo la kuvipiga vita vizuri vya imani mchungaji kanemba alinukuu kitabu cha yuda 1:2-4 na kusema kuwa imani wwaumini wamekabidhiwa mara moja tu ila tayari  ndani ya kusanyiko kuna watu ambao sio wa imani hiyo ila wameejiingiza ndani ya kundi kwa lengo la kuharibu kundi na kumwaga sumu.
Akifafanua zaidi lisema kuna kundi la watu wapo makanisani ila wanajaribu kupotosha imani ya kweli hasa pale ambapo somo la matoleo likianza kufundishwa wao huingilia kati na kuwaambia watu wasitoe sadaka huku yeye mwenyewe  hatoi sadaka ndani ya kusanyiko.
 Askofu Geofrey Massawe katikati kulia mchungaji wa Magomeni TAG  na kushoto mchungaji Oliva Massawe kwenye ibada.

 Mchungaji Dunstan Kanemba akimtambulisha mchungaji Mary Kanemba(mke wake) ambaye ni mchungaji msaidizi katika kanisa la Magomeni TAG.
 Mchungaji Mary Kanemba akisalimia waumini ambao hawapo pichani katika kanisa la TAG Mabibo Sahara siku ya jumapili ya tarehe 25 may 2014 na pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili.
 Mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Magomeni mch.Kanemba ndani ya madhabahu ya Mabibo TAG Sahara.





 Waumini wa kanisa la Mabibo Sahara TAG wakifuatilia neno kwa makini wakati mchungaji Kanemba hayupo pichani akifundisha kanisani.

 Baadhi ya viongozi wa kanisa la Mabibo Sahara TAG wakifuatilia neno kwa makini katikati mwenye tai Dr Shilla.
Mara baada ya ibada ya neno kuisha shughuli rasmi ya kutangaza uchumba wa kijana wa mwisho wa askofu Geoffrey Masawe ikaanza shangwe mnderemo na vivijo vilitawala ndani ya kanisa kwa wakati ule wa kutangaza uchumba.
Mgeni ambaye amealikwa kwa shughuli hiyo maalum si mwingine nia mchungaji Kanemba ambaye amesindikizwa na mke wake Mary.


 Ndugu Ebenezer Geofrey Masawe akisimama na mshenga wake wakati wa kutangaza uchumba kanisani.
 Miss Tumaini akiwa na mpambe wake ambaye amemsindikiza.
 Hapa sasa ndiyo penye shughuli una nini cha kudhibitisha kijana hakuchelewa alizama mfukoni na kutoa pete inayong'a na kumvisha miss Tumaini tayari kumbukumbu.
Miss Tumaini hakuchelewa kuonesha kidole kwa mapaparazi na waumini  kwa uso wa furaha.
Kazi ikabaki kwa Watumishi wa MUNGU kuwaweka mbele za MUNGU kwa hatua ambayo wameianza ili yeye mwenye uwezo na mamlaka awatangulie katika safari kwa huwa wengi wanshindwa kufikia lengo.

Waumini wakiifuatilia zoezi kwa makini wakiwa na nyuso za furaha.
 Karibu mwanangu utakuwa rafiki yangu wa karibu.

 Mr Ebenezer akiwa katika picha ya pamoja ndani ya kanisa na miss Tumani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni