YESU NI JIBU

Alhamisi, 15 Mei 2014

KUTAMBUA NA KUFAHAMU AINA 12 ZA WATU WASUMBUFU KATIKA JAMII!

Ungana na mtumishi wa MUNGU mchungaji Peter Mitimingi katika ufafanuzi wa aina 12 za watu wasumbufu katika jamii nawe utafakari kuwa upo kwenye kundi gani kati ya makundi hayo 12.

Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa Voice of Hope Ministries (VHM).

Utangulizi
• Katika kila watu 10 kuna vichaa 2
• Kuna watu wanakwaza mpaka hautamani kuishi nao
• Hao vichaa 2 wamewekwa maalumu ili kukushughurikia usije ukaota kiburi.
Katika jamii tunayoishi sasa kuna aina na makundi mbalimbali ya watu. Kunawengine ni waungwana sana, wengine wakorofi sana, wenye tabia nzuri na wenye tabia mbaya pia.


AINA YA KWANZA
SPONJI

1. Kazi kumbwa ya mtu wa aina hii ya sponji kama unavyojua sponji kazi yake ni kufyonza tu mara inapowekwa kwenya maji huachukua maji kutoka kwenye bakuli na kuyahamishia kwake.

2. Mtu huyu wakati wote ana uhitaji, lakini kamwe hatoi kitu kwako. Anasema chako ni changu na changu ni changu.

3. Ni mtu anayetumia vitu na mali za watu wengine kwa manufaa yake binafsi na kamwe hawezi kuwaza wala kupenda kutoa vyake kwa wengine.

4. Anataka yeye tu, ndiye wapewe. Asipopewa anakuwa mkali na lawama nyingi na wakati mwingine kususia jambo fulani. Lakini yeye asipotoa anataka aeleweke na ichukuliwe kuwa ni bahati mbaya hajatoa na ni kawaida tu. (mambo madogo)

5. Huwa hatoi sadaka wala mafungu ya kumi kanisani wala michango yeyote ya harusi au jumuiya fulani. Neno SINA kwake ndio kama wimbo wa taifa anauimba kila iitwapo leo.

6. Yeye anapokuwa na jambo linalomhusu, huwa wakwanza kuchangisha na kudai michango hata kama ni kwa nguvu atataka achangiwe au asaidiwe tena kwa haraka bila ya kucheleweshwa.

7. Wakati mwingine hudai michango kana kwamba niyeye aliye kukopesha kumbe ni msaada au mchango anadai kwa nguvu na vibaya mpaka inakuwa kero kwa yule anayetaka kumchangia au kumsaidia.

8. Sponji hujihalalishia kwamba yeye ni maskini hivyo anakibali maalum na sababu nzuri za kutokutoa. (Excuses)

9. Sponji Haina Uwezo wa Kutunza Maji Iliyoyanyonya Chomboni
Mara nyingi sponji inaponyona maji kutoka kwenye chombo, ukiitoa nje ya chombo huwa haina uwezo wa kuyatunza yale maji iliyoyanyonya kutoka kwenye chombo na kuyahifadhi, badala yake yale maji hudondoka na kupotea kabisa.

Ndivyo alivyo mtu huyu aina ya Sponji hata kama atapata pesa na mali kwa kunyonya kwa wengine mara nyingi ni watu wasio na maendeleo kabisa kwani huwa hawana uwezo wa kutunza na kumiliki vile walivyoweza kunyonya kutoka kwa wengine.

10. Sponji ni mtu maarufu sana kwa kukopa na kamwe halipi deni. Ukikomalia kumdai urafiki wenu unaishia hapo na pia hatakulipa kabisa.
sasa nawe jichunguje je upo kwenye kundi hi la kwanza ama katika mukundi kumi na moja yaliyosalia.
ya ni kutoka kwa mwalimu,mchungaji  Peter Mitimingi mk urugenzi wa VHM

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni