YESU NI JIBU

Jumanne, 20 Mei 2014

HALI YA TOFAUTI YAIBUKA MARA BAADA YA WANAWAKE WA ITALIA NA WENGINEO WAKITAKA MAPADRE WAPEWE KIBALI YA KUOA.



Wanawake washindwa kuzuia na kuficha hisia zao kwa mapadre na kuamua kuweka bayana kuwa ni vyema nao wakapata kibali cha kuoa.
Haya yametokea bada ya wanawake zaidi ya 26 kutaka kuwa na mahusiano na mapadri kitu ambacho hakijawaki kuwepo sasa wao wameona kuwa ni vyema wapewe ruhusa ya kuoa.
Papa Francis kiongozi wa kanisa katoliki.
Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.
Wanawake hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao wako katika hali kama hiyo.
Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa useja,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita. 
sasa nawe msomaji unasemaje kuhusu ssakata hilo unaweza ukatoa maoni yako. 
                                          habari chanzo BBC.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni