YESU NI JIBU

Alhamisi, 22 Mei 2014

MAADHIMISHO YA MIAKA 75 KATIKA KANISA LA TAG MABIBO SAHARA


Taasisi mbalimbali zimetakiwa kujitikeza kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalum( utindio wa ubongo) kwa kuwapatia misaada mbalimbali itakayo wasaidia katika maisha yao ya kila siku.
Kauli hiyo imetolewa na askofu wa jimbo la mashariki kaskazini na pia ni mchungaji kiongozi wa Mabibo Sahara Spritual Center askofu Geoffrey D Massawe wakati akikabidhi msaada wa vitu vyenye thamani ya lakini lane kwa watoto wenye uhitaji maalum katika shule ya msingi Mabibo jijini Dar es salaam.
Akielezea juu ya kutoa msada huo askofu Massawe alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo wakati wa maadhimishyo ya miaka 75 ya kuwepo kwa kanisa la Tanzania Assemblies of God hapa nchini na pia kuwepo kw a kanisa hilo katika maeneo ya mabibo.
Aidha akisoma risala kwenye sherehe hiyo ya maadhimisho ya miaka 75 askofu Massawe alisema  kanisa hilo lilianza kama tawi la kanisa la Ubungo Christian Centre mnamo September 16, 2001 likiwa na idadi ya washirika wanne chini ya uongozi wa wake akishirikiana na mke wake Mchungaji Olivia Massawe na Mchungaji Blanca Shayo kama wachungaji wasaidizi. Kanisa hili lilianzishwa katika mazingira magumu na katika eneo finyu ambalo awali lilikuwa gereji.

“Wakati wa kuanzishwa kwa kanisa hili nlikuwa mfanyakazi wa serikali katika mamlaka ya bandari. Kwa kumheshimu Mungu nifanya maamuzi ya kuacha kazi na kuanza kumtumikia Mungu (Full Time Minister). Sio mimi tu aliyefanya maamuzi ya kuacha kazi, ila na mke wangu mpenzi Mchungaji Olivia aliyekuwa mfanyakazi wa serikali naye aliacha kazi na kuamua kumtumikia Mungu. Maamuzi haya hayakuwa rahisi ila tulimwamini Mungu kuwa ataitunza familia yetu, maana tualikuwa na watoto ambao bado walikuwa wanawategemea sana”alisema askofu Massawe.
Kwa muda wote wa miaka tisa tulikuwa katika jukumu la kutafuta kiwanja,mara kadhaa Mungu alituepusha kuangukia katika mikono ya matapeli waliotaka kutuuzia viwanja vyenye matatizona mwishowe kabisa ndipo tulipopata kiwanja hiki ambacho kilikuwa kinauzwa milioni 100, ila kwa neema ya Mungu kiligharimu milioni 60 na kiwanja cha hekari mbili ambacho kilikuwa mali ya yangu na familia. Na tukabaini kuwa tatizo kubwa walilonalo makanisa mengi mijini hasa Dar es Salaam ni upatikanaji wa viwanja na gharama kubwa za manunuzi.
Hata hivyo alisema kuwa ujenzi wa kanisa hili haukuchukua muda mrefu  ulichukua takribani miezi mitatu na kwa sababu hiyo tunamshukuru sana Mungu aliyetujalia viongozi na washirika wenye moyo mzuri na utayari wa kufanya kazi ya Bwana, tunajivunia sana viongozi na washirika wa kanisa letu kwani waliwezesha ujenzi wa kanisa hili kwa miezi mitatu bila msaada kutoka nje.
Pamoja na hayo Ujenzi wa kanisa hili umekuwa katika awamu mbili, ya kwanza ya umekamilika, na gharama awamu ya kwanza ni shilingi milioni 120 na katika awamu ya pili  ni  upanuzi na tumekusudia kuongeza jengo hili kwa kuelekea kusini (eneo la madhabahuni). Katika awamu hii tutavunja jengo dogo lenye ofisi ya Mchungaji na tutajenga ghorofa tukiunganisha na kanisa. Baadhi ya ofisi zitakuwa ghorofani na eneo la chini litakuwa sehemu ya kuabudia na tumeanza maombi na katika siku za usoni tutaanza kukusanya pesa kwa kusudi hili,kwani  itagharimu shilingi milioni sabini (70).
Askofu Massawe hakuwa nyuma kuelezea  changamoto nyingi ambazo walikutana nazo tangu mwaka 2001 hadi leo,ila hazikutuzuia kufanya kazi ya uinjilisti. Pamoja  na uchanga na udogo wa kanisa hili bado tulilipa agizo kuu la Bwana wetu Kristo kipaumbele.  Kanisa hili likiongozwa na idara ya uinjilisti tangu mwaka 2002 hadi leo limeweza kufanya mikutano ya injili maeneo tofauti ya nchi yetu ya Tanzania. Na maeneo mengine tumefanikiwa kuanzisha kazi mpya au kufanya ujenzi wa majengo ya makanisa kama ifuatavyo. Mwaka 2002 tulifanya mkutano Malolo Mbozi, mwaka 2003 Mabamba Kibondo, mwaka 2004 Mwisenge Msoma, mwaka 2005 Igowole Mufindi, mwaka 2006 Bugango Bukoba, mwaka 2007 Kicheba Mheza, katika eneo hili la Kicheba hapakuwa na kanisa kabisa, hivyo baada ya mkutano tulianzisha kanisa. Mwaka 2008 tulifanya mkutano Ludewa Iringa, na baada ya mkutano tulifanya ujenzi wa jengo jipya la kuabudia. Mwaka 2009 tulifanya mkutano Esonge Kilindi, mwaka 2010 tulifanya mkutano Mhoro Rufiji na tumejenga nyumba ya mchungaji na kuweka umeme wa jua (Solar Energy Power), na 2012 tulifanya mkutano Mchukwi Rufiji, Kimara na Chalinze na mwaka 2013 tulifanya mkutano Bagamoyo eneo la Kiwangwa na baadaya ya mkutano tulishiriki katika ujenzi wa kanisa hilo. Vile vile tulifanya mkutano mwingine Ngerengere Eneo la Mliligwa na kufanya ujenzi wa kanisa, pia pamoja na ujenzi tunamtegemeza Mchungaji wa kanisa hilo kila mwezi.
Kanisa hili limekuwa na mkakati wa kutegemeza watumishi mbalimbali ili waweze kumtumikia Mungu kwa upendo na kwa kupenda. Miongoni mwa makanisa ambayo yanategemezwa ni kama yafuatayo:
·        Muhoro – Rufiji, kanisa lilimjengea nyumba Mchungaji wa kanisa hilo.
·        Kanisa la Utete – Rufiji
·        Kanisa la Gairo – Morogoro
·        Kanisa la Mlilingwa - Ngerengere
·        Mmishenari Madagascar
·        Vile vile tulimnunulia pikipiki mwangalizi wa Chalinze kwa gharama ya 1,950,000/= Ili kumwezesha kusimamia shughuli zake za uangalizi.
·        Kanisa la Goba, Matosa na
·        Kanisa la Temboni-Kimara

Tumeamua kuipa kazi ya Mungu kipaumbele.  Hivyo tumekusudia kuanzisha makanisa matatu eneo la Chalinze, Kibaha na Bagamoyo, na tumefanikiwa kuanzisha mawili bado kanisa moja. Pia tumeamua kuyasaidia makanisa matatu ambayo hayapo katika hali nzuri yanahitaji msaada wa haraka ili yaweze kuendelea. Makanisa hayo ni TAG Miswe, TAG Boma Maji lililopo karibu na mtambo wa maji ya Ruvu chini, na TAG Matimbwa.
Kwa kuhitimisha askofu Massawe alimshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufikia mafanikio haya na kukiri kwamba Mungu ametusaidia, anatusaidia na atazidi kutusaidia. Mungu ataitetea kazi yake sio tu hapa Sahara na popote pale ulimwenguni. 
 
 Askofu massawe akiwasili kwenye shule ya watoto wenye uhitaji maalum.
 Askofu Geoffrey na mchungaji Oliva Massawe wakifurahia ibada ya maadhimisho ya miaka 75 ya kanisa la TAG katika kanisa la mahali pamoja Mabibo Sahara.

 
 
 
 
 Askofu Massawe akitoa bidhaa ambazo wametoa kwa watoto wenye mahitaji maalum huku diwani na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo wakishuhudia.
 Katibu wa kanisa TAG Sahara ndugu Nikas akifafanua gharama ya bidhaa ambazo wametoa kwa watoto wenye mahitaji maalum.






Hakuna maoni :

Chapisha Maoni