YESU NI JIBU

Alhamisi, 15 Mei 2014

MUNGU AMEWEKA KARAMA MBALIMBALI KWA WATUMISHI ILI KUTOA MAFUNDISHO NA ELIMU JUU YA MAISHA YA KILA MWANADAMU ILI UKIKUTANA NA HAYO USISHANGAE

  ZIFAHAMU AINA 12 ZA WATU WASUMBUFU KATIKA JAMII!SEHEMU YA PILI
Kutana na mkurugenzi wa huduma ya Voice of Hope(VHM) mchungaji Peter Mitimngi kwa ajili ya ufafanuzi wa aina 12 za watu wasumbufu katika jamii na bila shaka nawe msomaji utajitathimini kuwa nawe upo kwenye kundi gani na hapa mchungaji Mitimingi ameandika kwa kufafanua.


Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa huduma ya The Voice of Hope Ministries (VHM).
AINA YA PILI
MKUSANYA TAKATAKA (Mama PekuPeku) GABAGE COLLECTOR

1. Mtu huyu hujiweka katikati ya watu wasio sahihi na wenye hali za moyo zilizoharibika.
2. Mtu huyu ni kama nyoka, mnyama mwenye sumu kali sana ambapo akikugonga sumu yake huweza kuenea kwa kasi sana katika mwili wa mwanadamu na kwa haraka.
3. Mkusanya takataka ni mtu mzushi na muongo anayependa kusambaza uongo na uzushi. Mambo asiyoyajua yalikotoka wala yanakokwenda.
Zaburi 52:3
Umependa mabaya kuliko mema, Na uongo kuliko kusema kweli.
4. Kipaumbele chake cha kwanza ni kusengenya na kutapanya uongo na uzushi wenye sumu kali ya kuangamiza na kugombanisha watu.
5. Mara kwa mara hutumia muda mwingi kuzunguka zunguka kutafutiza maneno ya uzushi,uongo na umbea na kuchonganisha watu.
Mithali 14:5
Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.
6. Mbeba takataka (mama pekupeku)Hata Pumzi yake akipumua imejaa Uwongo Mtupu.
7. Siku zote huyasema madhaifu na mapungufu ya wengine, kamwe hawezi kuyasema yale yanayo muhusu yeye.
8. Hupata nguvu ya kuzungumza na kuyasema hayo maneno ya wengine wakati ambapo mhusika anapokuwa hayupo. Mara mhusika akiingia kwa bahati mbaya, basi maelezo yake huishia hapo hapo au hubadilisha mada kwa ghafla na kujichekesha chekesha kwa muhusika aliyekuwa anamsengenya.
9. Ni kama chura ambaye yupo majini hulia na kupiga kelele nyingi lakini ukitupia jiwe moja tu, ananyamaza kimya kama vile hakuna kelele. Ndivyo alivyo huyu mama peku peku.
10. Hawezi kujisikia raha wala amani kama hajaongea uongo au mambo ya uzushi. Kuzusha na kuongea maneno ya uongo kwake ndio burudani. Kama hakuna hayo maneno yupo tayari hata kutembea umbali mrefu kwenda kukusanya na kutafutiza umbea ili aweze kuusambaza.
Usoma aina ya kwanza kwa umakini sasa sehemu ya pili maana aina ya pili umeifahamu zaidi ya yote usikose aina ya tatu na kwa sasa umejitambua kuwa upo ama haupo kwenye kundi la aina ya kwanza na ya pili endelea kusoma ili kupata maelezo juu ya aina hizo zingine kumi zilizosalia



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni