YESU NI JIBU

Jumapili, 11 Mei 2014

UKIJISHUSHA KWA MUNGU,YEYE HUKUINUA KWA WAKATI WAKE

Ukimtumikia MUNGU kwa uaminifu hukuinua katika wakati wake maana yeye ni mwaminifu na hafananishi na yeyote usemi huu umedhiirika kwa mchungaji msaidizi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God  Kinondoni mchungaji Christopher Mlaponi kwa kusimikwa kuwa mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG makongo poters house lilopo makongo juu.
Akimsimika mchungaji Mlaponi askofu wa jimbo la mshariki kaskazini askofu Geoffrey Massawe alisema kuwa ni vyema kumtumikia Mungu kwa roho na kweli na kanisa nalo lisimamie kuwasaidia watumishi wa Mungu ili kazi yake iweze kusonga mbele.
Akizungumza mara baaada ya kusimikwa mchungaji Mlaponi aliendelea kuwaasa viongozi wa dini jamii na wanasiasa kuwa na upendo maana bila upendo hakuna kitakachoendelea.
Aidha alisema kuwa viongozi wa serikali kutumia nafasi zao vizuri kwa uaminifu ili kuwasaidia watanzania kufanikiwa hasa kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku.
  Askofu wa jimbo la mashariki kaskazini  askofu Geofrey Massawe akihubiri wakati wa kumsimika mchungaji Christopher Mlaponi.


 Askofu Massawe mwenye suti nyeupe mara baada ya maombi kwa mchungaji Christopher.
 Waumini wakishiriki maombi ya kumweka wakfu mchungaji Mlaponi kuwa mchungaji kiongozi.
  Haya sasa picha ya pamoja na viongozi wa kanisa.

  Mchungaji Mlaponi akiwa amekaa kwenye picha pamoja na watoto kanisani mara baada ya kusimikwa.
 Ni kusalimiana na washira wake katika kanisa jipya.
 Mara baada ya huduma ya kuweka wakfu sasa ni wakati wa kula,askofu Massawe akichukua chakula.

 Ni wakati wa kujumuika pamoja ,tufurahini maana ni Bwana.



  Hili ndilo kanisa la poters house TAG makongo juu ambalo kwa sasa mchungaji mlaponi amesimikwa kuwa mchungaji kiongozi rasmi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni