YESU NI JIBU

Jumatatu, 7 Machi 2016

ZIFAHAMU DALILI SABA ZA NDOA INAYOELEKEA KUVUNJIKA NA MWALIMU NA MCHUNGAJI DK PETER MITIMINGI NI SEMINA YA NDOA AMBAYO IMEFANYIKA KATIKA KANISA LA MORAVIAN DAR ES SALAAM!

Mchungaji na mwalimu Dk mitimingi akifundisha katika semina.

Hizi ni dalili ambazo zinaashiria kuwa ndoa inaelekea kuvunjika,pale utakapobaini kuwa mwanandoa
1. Wakati wanandoa wanapokuwa hawaongei tena kila mmoja kwa mwenzake. (Partners no longer talk to each other).
2. Wakati wanandoa hawaonyeshi tena matendo ya mapenzi kama vile Kukumbatiana, kushikana mikono, kumbusu mwenzi wako, na kuonyesha kumjali mwenzi wako. (They no longer hold hands, kiss, or careless).
3. Wakati ambapo maisha ya UNYUMBA yanakuwa ya kuchoshana na hayana ladha wala raha tena. (Their sex life is boring).
4. Wakati ambapo kila mazungumzo yenu huishia kwenye kugombana na kununiana. (Every discussion or disagreement escalates into a major fight). Mnaanza vizuri kuongea mnaishia kulumbana na kugombana.
5. Wakati kila mmoja anampuuzia mwenzake na kuona hana mvuto tena. (They take each other for granted and no longer take time to look attractive).
6. Wakati ambapo wanandoa hao huachia muda wao mwingi kuchukuliwa na: 
• Wanandugu
• Marafiki
• Watoto
• Vitu kama kazi, biashara, kuchukua nafasi kubwa ya mapenzi ya wanandoa hao. (They let other people (relatives, children, 
or even things like jobs) come between them).
7. Wakati wanandoa hawafanyi tena mipango pamoja, kila mwanandoa kivyake vyake. (They no longer do things together any more).
Kama ukiona kuna dalili hizo katika ndoa yako basi anza kuchukua hatua na tahadhari mapema kabisa kuinusuru ndoa yako.
Mungu hapendezwi na wanandoa wanaofanyiana mambo ya hiana.
Malaki 2:14
14 Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
hizo ni dalili ambazo mwali na mchungaji Dk Mitimingi ameziandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii facebook.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni