YESU NI JIBU

Alhamisi, 10 Machi 2016

JUKUMU LA WATOTO WA KIKE KUPATA ELIMU NI LA JAMII KWA UJUMLA ALISEMA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR TULIA.

 Askofu Geofrey Masawe wa kanisa la TAG Spiritual Center 
Mabibo.
Naibu Spika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Tulia Akson ambaye hakuvaa sare wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wa kanisa la Sahara Spiritual Center.
 Askofu Geofrey Masawe akikabidhiwa zawadi na katibu wa wanawake kulia ni mchungaji Manyama. 

Mchunaji Manyama akitoa matangazo katika siku ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi wa tatu.




Kwaya ya wanawake wakitumbuiza katika maadhimisho ya siku yao.
 Baadhi ya waumini wakifurahi kanisani hapo wakati wa kusifu.
 Waumini wakifuatilia kwa makini sherehe.
 Mwimbaji wa njimbo za injili Jeniffer Mgendi akiimba katika sherehe ya wwk katika kanisa la Sahara Spiritual Center Mabibo.
 Viongozi wa akina mama wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu Masawe pamoja na mchungaji manyama.


Imebainika kuwa kuna mabadiliko makubwa ndani ya jamii kuwa jukumu la kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapata elimu ili wafikia malengo yao na kuwa na fursa na nafasi mbalimbali pamoja na, kuwepo kwa changamoto zinazowakabili katika maisha yao.
kauli hiyo imetolewa na naibu spika wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe.Dr Tulia akson wakati akizungumza na na gazeti la jibu la maisha katika kanisa la sahara spiritual center  jijini Dar es salaam,ambapo alisema kuwa jamii imebadilika sana na wanawake wamepata fursa ya kupata elimu pamoja na jamii kuwa na mategemeo makubwa kwa mwanamke.
"Mpaka sasa wanawake wamekuwa na nafasi mbalimbali ndani ya jamii serikalini pamoja na katika mashirika mbalimbali ila bado suala la ukandamizaji kwa wanawake na watoto wa kike bado unaendelea ila inahitajika kuwepo na jitihada na juhudi za kumsaidi  mtoto wa kike na mwanamke ili wawe huru na kupewa majukumu sawa na wale watoto wa kiume ama wanaume wanapewa alisema",mhe.Dr Tulia
Aliwasihi wanawake kuwa na hekima na busara katika familia zao hasa
Hata hivyo alisema kuwa jamii italazimika kubadilika kuendana na muda na mazingira ya teknolojia na aliwasihi wanawake kumwomba Mungu awajalie  hekima na busara ili waweze kuishi na waume zao katika mazingira yote.
Na kwa upande wake askofu wa jimbo la mashariki kaskazini na pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Mabibo Sahara Spiritual Cente Askofu Geofrey Masawe katika maadhimisho ya sherehe ya siku ya wanawake watumishi wa kristo wwk alisema kuwa ukandamizaji na unyanyasai kwa wanawake inaonekana kama ni hali ya kihistoria ambayo imewaumiza na kuwafanya wanawake kuonekana kuwa duni na kubaguliwa.
.
Aidha Askofu Masawe aliongeza kuwa kila jambo linawakati na majira yake hivyo jambo la ukandamizaji wa wanawake umekuwepo kwa nyakati za mwazo ila kila kukicha kunakuwepo na mabadiliko.
Naye mkurugenzi wa wwk Sahara Spiritual Center Isabela Ngonya alisema kuwa wao kama wanawake watumishi wa kristo wamejikita katika kusaidia jamii inawazunguka na wenye mahitaji mbalimbali ili waweze kupata mabadiliko.
aliongeza kuwa wao kama wanawake watumishi wamejitolea kuwasaidia watumishi na kufikishia injili kwa wasiofikiwa ambayo ni mikakati chama cha wwk.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni