Hatimaye
Jumamosi ya tarehe 19 Kyela, ndipo mwili wa Mama Frida Mwamwaja ulipumzishwa,
baada ya kufariki tarehe 15 Machi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mama Frida amezaliwa tarehe 19 Disemba 1953, hivyo kufariki akiwa na umri wa
miaka 62 akiacha watoto 3 wa kiume na mmoja wa kike, huku wajukuu wakiwa saba.
Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto mmojawapo wa marehemu, kwa ghafla akiwa chumbani
kwake alianza kusikia kizunguzungu, na baada ya hapo alianza kuomba na kisha
alipomaliza alipata wakati mgumu kupumua na kisha kuanguka, kabla ya kuwahishwa
hospitalini kwa ajili ya uangalizi zaidi, hadi hapo mauti ilipomfika.
Ksatika yote, hatuna cha zaidi ya kumtukuza Mungu kwa ukuu wake,
maana atenda na kuwaza kwa muda wake tofauti na wanadamu. Tunaomba faraja ya
Mungu iwe pamoja na wafiwa wote, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki popote pale
walipo.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA libarikiwe.
kwa idhini ya gospelkita
Mama Frida amezaliwa tarehe 19 Disemba 1953, hivyo kufariki akiwa na umri wa miaka 62 akiacha watoto 3 wa kiume na mmoja wa kike, huku wajukuu wakiwa saba.
Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto mmojawapo wa marehemu, kwa ghafla akiwa chumbani kwake alianza kusikia kizunguzungu, na baada ya hapo alianza kuomba na kisha alipomaliza alipata wakati mgumu kupumua na kisha kuanguka, kabla ya kuwahishwa hospitalini kwa ajili ya uangalizi zaidi, hadi hapo mauti ilipomfika.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA libarikiwe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni