YESU NI JIBU

Jumatatu, 28 Machi 2016

MWENYE MACHO NA MASIKIO ASIKIE NA KUFAHAMU KUWA ULIMWENGU UNAELEKEA UKINGONI:


Ni nyakati ambazo kila mwanadamu anatakiwa kuwa makini na kuangalia kinachoendelea katika ulimwengu wa mwili na hata wa roho.
Katika ulimwengu tunamoishi kwa sasa kuna mambo mengi yanaibuka kila kukicha ambapo wanadamu wengi wanajiita mungu na wengine wameanza kuabudiwa lakini mwisho wake wanakufa na kupoteza maisha jambo ambalo kwa wengi wenye imani ya kweli hufahamu na kutambua kuwa ni nyakati za mwisho.




 Hivi ndivyo jengo la kanisa ya Beyoce invyoonekana kwa nje.
Kitabu ambayo hutumiwa na waumini wa beyism,
Akizungumza na blog hii mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center askofu Florian Katunzi amesema kuwa 
kwa mujibu wa maandiko matakatifu mtu ajifanyaye Mungu ni nabii wa uongo,ambaye anatumikia roho ya mpinga kristo,
Aidha ukimfuatilia kwa makini mwanamziki huyo Beyonce utagundua kuwa yupo kwenye mtandao wa waabudu shetani kwa matendo yake na ishara zake zinaashiria kuwa anaabudu shetani kwa mujibu wa maandiko matakatifu utabaini katika kitabu cha 1yohana 2:18 -19 
18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 
19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 

Moja ya picha ambazo ni alama za freemason ambazo Beyonce amekuwa nazo.




Hii sio ya kushangaa maana kila mwanadamu anakuwa na mawazo yake na kuamua kujiinua mwenyewe jambo ambalo ni kosa hasa kuta kuabudiwa kama Mungu.

Katika ulimwengu wa sasa kuna  kanisa jipya linanoitwa 'The national church of Bey'
Kanisa hilo limeanzishwa na Msanii Nguli wa Muziki duniani Beyonce Knowles raia wa Marekani ameacha maswali mengi baada ya kuanzisha kanisa lake na kuliita "The national church of Bey" means church of Beyonce, ambapo yeye ndio Mungu wa kanisa hilo na maelfu ya watu wanamuabudu kwa jina la "mother Bey"
Katika kànisa hilo kuna picha ya Beyonce akionekana na Vazi la yesu, na nyingine akiwa na vazi LA papa wa dhehebu LA RC. 
Amekuwa akiitwa Mungu wa kike.. Na dini yake inaitwa "Beyism" ambapo pia wanatumia biblia yao inayoitwa Beyble, inamzungumzia Beyonce kama mwanamke mwenye uwezo wa ajabu kama Mungu na kuamua kumuita Goddess..
Dini hiyo ya Beyism ina waumini maelfu ambapo inaonesha baadhi ya wafuasi wa Mungu huyo Beyonce, watu maarufu kama Kanye west, Mariah carrey na wengine.
Mwenye masikio na alisikie na kulifahamu neno na kufuata ukweli waa neno la MUNGU na Imani ya kweli.
MASOMAJI WETU TUPE  MAONI YAKO NA KAMA UTAKUWA NA HABARI JAMBO UNAWEZA KUWASILIANA NASI KWA EMAIL AMA KWA SIMU 0682672828.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni