YESU NI JIBU

Jumatano, 16 Machi 2016

MHE. PAUL MAKONDA AMSHUKURU MUNGU KUMTIA NGUVU KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA UKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM:

 Mh. Paul Makonda akiwa na Mke wake akimshukuru Mungu
Ilikuwa ni Jumapili ya namna yake baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kufika katika ibada ya jumapili na kutoa shukrani katika kanisa la Living water makuti kawe kwa mtumishi Apostle Onesmo Ndegi.

Mapema akimkaribisha kuzungumza Mhe. Paul Makonda Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mh.Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake.

Baada ya Ibada hiyo ya shukrani Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Hongera Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mh. Paul Makonda wakati akizungumza ndani ya kanisa la living water makuti Kawe
Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi 
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda

 Mh. Paul Makonda akifafanua jambo
Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini
Apostle Onesmo Ndegi, Mke wake Lilian Ndegi na Mch. Peace Matovu wakifanya maombi kwa Bwana na Bibi Makonda



Apostle Onesmo Ndegi,Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe akifanya maombi kwa watu waliokuja mbele kuokoka katika ibada hiyo
maombi kwa watu waliokuja mbele kuokoka katika ibada 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni