YESU NI JIBU

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

WATU SABA WAMEUAWA KINYAMA NA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO:

Ndugu msomaji wa blog hii hivi karibuni Askofu mkuu
wa wapo mission International Askofu Sylvesta Gamanywa amekuwa akifundisha juu ya suala la uchawi na kuelezea kwa umakini na Ukomo wa nguvu za uchawi katika kuigiza miujizambalimbali ndani ya jamii(KUT. 8:16-19)
baada ya hapo sasa fuatilia kisa hiki ambacho kimetokea huko mkoani kigoma ni vyema watu wa MUNGU kuwa macho maana nyakati tulizo nazo ni za hatari sana ubinadamu uko wapi kama binadamu anaweza kumuua mwenzake kwa kumchoma moto na kuteketeza makazi yake


Huu ndiyo unyama ambayo umefanywa na baadhi ya wanankijiji kwa kuteketezwa kwa moto nyumba na watu katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma









Hizi ni miongoni mwa nyumba20 zilizoteketezwa kwa moto katika kijiji cha Murufyiti wilayani Kasulu mkoani Kigoma
 Watu saba wameuwawa kikatili kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali kwa kuhusishwa na imani za kishirikina,huku nyumba ishirini zikichomwa moto katika kijiji cha Murufyiti,wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.


 Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma,Japhari Muhamed alisema,tukio hilo lilifanyika juzi majira ya saa nne usiku baada ya M/kiti wa kijiji hicho aitwaye Evarist Ruhaya akishirikiana na mganga wa jadi,Faustino Ruchagula kupiga mbiu ya hatari ili kukusanya watu na kufanya unyama huo.

Amesema watu waliouwawa ni ,John Muvuma (68),Elizabeth Kaje (55),Dyaba Kitwe (55),Vincent Ntiyaba (42),Helman Ntabiloye (78),Redamta Mdogo (60) na Ramadhani Kalaliza (70) wote wakiwa ni wakazi wa kjiji hicho cha Murufyiti,pia nyumba18 zilichomwa moto na zingine mbili kubomolewa na kutimiza idadi ya nyumba ishirini
 ....kamanda Mohamed amesema,tayari watu kumi na tatu akiwemo mwenyekiti wa kijiji wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo na msako mkali unaendelea kuhakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani.
 Naye mtendaji wa kijiji hicho Ogeni Gaspa alisema kabla ya wauaji kuanza alipiga simu kwa OCD ili polisi waje kutuliza ghasia lakini gari hazikuwepo kituoni hivyo hali iliyopelekea Polisi kufika eneo la tukio kwa kuchelewa na kukuta mtu wa mwisho akiuwawa.
kwa upande wa mtoto mmoja wa marehemu,aliejitambulisha kwa jina la Josiphat John alisema wakati tukio hilo linaendelea kwa wazazi wangu alishindwa kutoka nyumbani kwake kwa hofu ya kudhurika lakini ilipofika alfajiri alikwenda kuangalia miili ya wazazi wake ndipo alipokuta imeteketezwa na moto...
Picha kwa hisani ya  Lydia Mapunda



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni