Watu
hujiuliza na bila kupata majibu na kusema utawezaje kufanya mambo mawili kwa
wakati mmoja ,ila wanashindwa kuelewa kanakwamba unapokuwa mchungaji lazima
utafundisha na unapofundisha ili mtu akuelewe lazima uwe mbunifu na namna ya kutochosha
waumini wako .
Mchungaji
Mwansasu ana wito na kazi ya mungu hivyo ni lazima atumie kipaji chake ya kipekee kipaji cha uimbaji na anakitumia ipasavyo awapo madhabauni na
baada ya kuona anakipawa cha uchungaji akaona si vyema kuacha kufanya kazi ya Mungu na awapo popote pale aachi kuimba na pia kuwa mchungaji ni vitu ambavyo
mtumishi wa Mungu ni wajibu kutumia vitu hivyo kwa wakati mmoja .
Aidha
ieleweke wazi sio kambwa nipo kimya huwa kila muda na siku haipiti bila
kuimba,na uimbaji wangu kutoa albamu pia sio jambo la kuamka na kukurupuka na
kukimbili studio ni jambo la kusema na Mungu nifanye nini katika hiki kipaji
ulichonipa kwa ajili ya nchi yangu na mkoa wangu hata katika mataifa mengine.
Ni jambo
la kila mwimbaji kukaa na kutafakari
unapotoka na unapokwenda na tujiulize kwa nini nyimbo za zamani hazipitwi na
wakati za injili na kizazi hiki
nicha kumuomba Mungu sana kwani tumekuwa tukiimba bila kujua nini tunakifanya
waimbaji wa injili tumejisahau na kusema ni utandawazi kumbe sivyo watu wamungu
tunapaswa kuwa ,hivyo tuwe na upendo na kurudi chini na kumtumikia Mungu
tusitafute pesa kwa kupoteza jamii katika maadili ya kumcha mungu ,bali
tutafute kwanza ufalme na kumjengea Mungu.
Na safari
hii nakuja kivingine huwa nina ndoto yangu ya maisha na ndiyo maana Mungu
ananitunza, nyimbo zangu natamani sana Mungu anisaidie kwa kuangali na
kuzitafakari ukisikiliza upate ujumbe na ni wakila mmoja wetu hivyo
yakupasa kufanyia kazi.
Kipawa ch uimbaji na uchungaji namshukuru Mungu kwa kutumia roho mtakatifu na
kwa kunitumia,
Mwaka
1998,Albamu yangu ya kwanza ilifahamika kwa jina la Tutatesa milele ikiwa na
ujumbe wa kuwainua wacha Mungu na kuwataadharisha wanaopenda dunia waache na
kumrudia mungu ikiwa na nyimbo nane .
Mwaka 2001
Albamu ya pili ,Umepoteza namba,inamaanisha mtu unaemtafuta Mume wa mtu au mke
wa Mtu aache mara moja
Mwaka 2005
Albamu ya tatu Msigombane,Niliona ni kama kuna wakati tutagombana Viongozi wa
dini katika huduma na katika dini ,upendo utatoweka katika madhehebu mbali mbali
na viongoza wa dini na yametimia katika Mwaka 2013 Hadi sasa mfano makanisa
kuchomwa moto mashehe kugombana amani inatoweka.
Mwaka 2010
Wosia wa baba .ninamaanisha kila unapoongea na
mzazi iwe mzazi wako au aliyekuzidi umri lazima anapokupa wosia usiupuuzie
mzazi maadili yake huwa yanatokea.
Na safari
hii kweli linatimia ukimuomba mungu Mwaka huu ninazindua Albamu yangu ya tano
inakwenda kwa jina la Nina ndoto yangu Mabano I have a dream,namaanisha kila
mtu ana ndoto yake duniani na zipo ndoto ndogo, ya kati, na kubwa,lakini wenye ndoto
kubwa wanamambo makubwa,na madogo
ni madogo,hivyo mwenye ndoto lazima awe na maadui.
Kipawa
changu cha kuimba ni kutokana na mazingira ninayopita na Mungu hunitumia kwa
kupitia uwezo wa Roho mtakatifu na hadi mimi mwenyewe najishangaa vinatoka wapi
na mwisho wa siku vinatokea.
Kufanya
mambo mawili kwa wakati mmoja ,uimbaji na mchungaji ni utaratibu unajiwekea
ratiba yako tena unaweza kufanya zaidi kutokana na wewe mwenyewe unavyojiwekea
utaratibu wako wa kazi ,na pia kuimba na kuubiri ni vitu vinavyoenda sambamba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni