TOKA
KATIKA KABURI LA DHAMBI,TABIRI JUU YA MAISHA YAKO UPATE KUSTAWISHWA
Neno la Mungu linasema “Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje
katika roho ya Bwana akaniweka chini katikati ya bonde nalo limejaa mifupa akanipitisha
karibu nayo pande zote na tazama palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda!
Nayo tazama ilikuwa mikavu sana. Akaniambia mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza
kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU wajua wewe. Akaniambia tena, toa unabii juu ya mifupa hii
uiambie enyi mifupa mikavu lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya tazama, nitatia pumzi ndani yenu nanyi
mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu nami nitaleta nyama iwe juu yenu na kuwafunika
ngozi na kutia pumzi ndani yenu nanyi
mtaishi nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi
Bwana. Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa hata nilipokuwa nikitoa unabii,
palikuwa na mshindo mkuu na tazama tetemeko la nchi na ile mifupa ikasogeleana mfupa
kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama kumbe!
Kulikuwa na mishipa juu yake nyama ikatokea juu yake ngozi ikaifunika juu yake
lakini haikuwamo pumzi ndani yake. Ndipo akaniambia tabiri, utabirie upepo,
mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi njoo kutoka pande za pepo nne Ee pumzi,
ukawapuzie hawa waliouawa wapate kuishi. Basi nikatabiri kama
alivyoniamuru pumzi ikawaingia wakaishi
wakasimama kwa miguu yao jeshi
kubwa mno. Kisha akaniambia mwanadamu,
mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli tazama wao husema, mifupa yetu imekauka
matumaini yetu yametupotea tumekatiliwa
mbali kabisa. Basi tabiri uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi tazama nitafunua
makaburi yenu na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu enyi watu wangu nami
nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana,
nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu enyi watu
wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi nami nitawawekeni
katika nchi yenu nanyi mtajua ya kuwa mimi Bwana nimesema hayo na kuyatimiza asema
Bwana” Ezekieli
37:1-14
MGUSO
WA KWANZA.
Kama ambavyo neno la utangulizi linaonesha tafsiri mbili
za kifo ambapo yaweza kuwa ni kifo cha kiroho ambacho mauti hupata mtu kwa
jinsi ya roho japo kimwili anakuwa mzima na akiendelea vizuri na maisha yake ya
kila siku. Mauti hii humpata mtu atendaye dhambi maana mshahara wa dhambi ni
mauti sawa sawa na neno hili, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa
milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” Warumi 6:23
Yesu Kristo yeye ni mkombozi aliye hai na amekuja apate
kumkomboa mwana wa Adamu toka katika mauti ya kiroho na kimwili na apate kuwa
hai tena, maana yake ni kuwa tukimwamini
yeye kuwa ni BWANA na mkombozi wa maisha
yetu basi yeye anatuweka huru mbali na mateso na dhambi.
“Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru na kuwa mbali na dhambi na kufanywa
watumwa wa Mungu mnayo faida yenu ndiyo kutakaswa na mwisho wake ni uzima wa
milele.” Warumi
6:22.Hivyo unapaswa kuokoka kwanza ndipo huruhusu Mungu akuguse kwa mguso wa pili na kukufungua katika vifungo vyote vinavyokuzunguka.
MGUSO
WA PILI.
Mguso wa pili unaonesha dhahiri ya kuwa hatuwezi kuendelea mbele huku tukiwafungua
wale waliofungwa vifungo vya giza , magonjwa,madeni,dhiki na mateso kama
wasipokuwabali mguso wa kwanza wa
ukombozi yaani kuokoka.
Hivyo kuokoka ni lazima maana ndilo tendo pekee la
kiimani lenye kuleta nguvu ya Kimungu na ondoleo la dhambi kwa mwanadamu.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee ili
kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16Na neno linazidi kuthibitisha ya kuwa , “Bali mtu asiye haki Mungu amwambia una nini wewe kuitangaza sheria yangu na kuliweka agano langu kinywani mwako? Maana wewe umechukia maonyo na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.Ulipomwona mwivi ulikuwaradhi naye, ukashirikiana na wazinzi. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya na ulimi wako watunga hila.Umekaa na kumsengenya ndugu yako na mwana wa mama yako umemsingizia.Ndivyo ulivyofanya nami nikanyamaza ukadhani ya kuwa mimi ni kama wewe. Walakini nitakukemea nitayapanga hayo mbele ya macho yako.Yafahamuni hayo ninyi mnaomsahau Mungu nisije nikawararueni asipatikane mwenye kuwaponya. Atoaye dhabihu za kushukuru ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, nitamwonyesha wokovu wa Mungu.” Zaburi 50:16-23
Katika Yesu tunaamini ya kuwa ndiye sadaka ya ukombozi kupitia damu yake iliyomwagika pale msalabani hivyo katika yeye tunapata uzima wa milele maana, “Na hilo alilinena ili kumjaribu kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda.” Yohana 6:6
Lazima mtu ukubali kwanza kuzaliwa mara ya pili ndipo
upate faida za ufalme wa Mungu katika Adamu wa kwanza tunakufa lakini katika Adamu wa pili tunahuishwa upya.
Kuhuishwa ni
kurejeshewa uzima na uhai maana Mungu atakulinda na kukuongoza sanjari na
kukutenga na wale waovu, “Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.“Zaburi 50:5
Lakini dhambi ni uozo wa kimaadili unaopingana na kweli
ya Mungu ndani mwa mwanadamu maana Adamu wa kwanza alipotenda dhambi , iliingia
kwa wanadamu wote. Lakini neema ya Mungu na kipawa chake cha ukombozi
kimefunuliwa kwetu kwa njia ya Yesu Kristo, ndio maana ni lazima mtu akubali
mwenyewe kuokoka ndipo uponyaji unafuata, japo wengi wanataka kuombewa na kufunguliwa
wakati dhambi zimejaa mioyoni mwao hapa panahitaji mtazamo sahihi kuhusu
dhambi.
“Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu, bali wenye haki ni
wajasiri kama simba” Mithali 28:1 Lakini BWANA anasema, “Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako ujana wako ukarejezwa kama tai” Zaburi 103:3-5
Anaongeza kuwa, “Maana yeye aliye juu aliyetukuka, akaaye milele ambaye jina lake ni Mtakatifu asema hivi nakaa mimi mahali palipoinuka palipo patakatifu tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea ili kuzifufua roho za wanyenyekevu na kuifufua mioyo yao waliotubu.” Isaya 57:15
Hivyo ni wazi kuwa toba inasababisha ufufuo wa kiroho na
kimwili maana BWANA anaziangalia njia za kila mtu ili apate kumlipa sawa na
njia zake, “Nimeziona njia zake
nami nitamponya nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake yeye na hao
wanaomlilia.” Isaya 57:18
Mifupa mikavu lazima ipate kuishi. Lazima kutoka katika
kaburi la dhambi,uzinzi na zinaa maana katika siku za leo hata wana ndoa
wanashindwa kupeana haki zao za msingi hivyo kuwafanya wawe na tamaa na kuangalia makahaba nah ii
inasababishwa na kuruhusu hali ya dhambi iingie mioyoni mwao, “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na
utukufu wa Mungu;” Warumi 3:23
Ni wazi kuwa peke yetu hatuwezi lazima tuhitaji msaada wa
Mungu ili tujazwe nguvu za kuangusha kila ngome na kila fikra ziinukazo juu ya kinyume
na matakwa ya Mungu.
Katika mguso huu wa pili lazima tutabiri juu ya wote waliouwawa kiuchumi,kiroho na
kimwili maana watarejeshewa tena kwa kufungua sanda zao zote za magonjwa,dhiki
madeni,uchungu moyoni, utasa na ugumba visitawale katika maisha ya wateule na hapa tunapata nguvu ya ufufuo na uzima katika Yesu Kristo.
“Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani
yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo
katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.” Warumi 8:11
Roho wa BWANA Mungu yu juu yangu ili kuwagusa na kuwafungua
wote waliofishwa na magonjwa katika miili yao wapokee uzima tele.
Na wale wenye dhiki katika maisha yao BWANA atayafunua
sasa makaburi yote kwani hiki ni kipindi
cha baraka na ustawi.
Umepoteza
matumaini BWANA anasema usiogope maana, “.....wao husema mifupa yetu imekauka matumaini yetu
yametupotea tumekatiliwa mbali kabisa. Basi tabiri uwaambie Bwana MUNGU asema
hivi tazama nitafunua makaburi yenu na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu
enyi watu wangu nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua
ya kuwa mimi ndimi Bwana nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa ninyi katika
makaburi yenu enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu nanyi mtaishi
nami nitawawekeni katika nchi yenu nanyi mtajua ya kuwa mimi Bwana, nimesema
hayo na kuyatimiza asema Bwana.” Ezekieli 37:11-14
Mguso wa pili ni nafasi nyingine ambayo BWANA ataitumia
ili kufufua makaburi ya kichawi yaliyofunga mabinti wasiolewe na yaliyofunga ndoa
za watakatifu zisiinuke tenana hakutakuwa na kufa wala kuzaa mapooza, “Watu wa
mjini wakamwambia Elisha angalia twakusihi mahali pa mji huu ni pazuri, kama
bwana wangu aonavyo lakini maji yake hayafai na nchi huzaa mapooza. Akasema nileteeni
chombo kipya mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda
mpaka chemchemi ya maji akatupa ile chumvi humo ndani akasema Bwana asema hivi
Nimeyaponya maji haya hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. Hivyo yale
maji yakapona hata leo sawasawa na neno la Elisha alilolinena.” 2Wafalme
2:19-22
Miradi ya
kuiuchumi na kazi za mikono zinafufuliwa maana, “Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha geukeni upande wa kaskazini.” Kumbukumbu la Torati 2:3Anawatia moyo ya kuwa , “Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako.” Mithali 23:11
Naomba sasa kwa ajili yako uisikie sauti ya mwokozi Yesu
iinuke kwenye vilio vyako vya maombolezo na minyonyoro iliyokufunga ifunguke
sasa.“Naye Mungu wa amani
atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na
iwe pamoja nanyi. [Amina.]” Warumi 16:20
Usiogope wala kukata tamaa, “Umtwike Bwana mzigo wako
naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele”.Zaburi 55:22Kwakuwa, “Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau” .Zaburi 51:17
Na BWANA atatoa kilicho chema, “Naam, Bwana atatoa kilicho chema, na nchi yetu itatoa mazao yake” .Zaburi 85:12
Lakini Mungu anataka tukubali kwa mioyo yetu wenyewe, “ Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga maana kinywa cha Bwana kimenena haya” Isaya 1:19-20
Mapinduzi lazima yafanyike sasa katika ulimwengu wa roho
upate baraka za rohoni na mwilini upate kuishwa tena kiroho, “Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu, Na kazi ya
mikono yetu utufanyie thabiti naam kazi ya mikono yetu uithibitishe” Zaburi
90:17
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni