Licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na
serikali pamoja na taasisi zisizo za kiserikali katika kuhamasisha na kupambana
na vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vitendo vya kikatili vinaendelea kujitokeza
katika jamii kadri siku zinavyoongezeka.
Tunapo zungumzia vitendo vya ukatili wa
kijinsia tunamaanisha kuwa ni pamoja na
vipigo kwa wanawake,wanaume kutelekeza watoto na familia zao,ukeketaji,ndoa za
utotoni,mimba za utotoni pamoja na
mauaji ya vikongwe.
Yapo
mashirika na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali ambazo
zimekuwa mstari wa mbele katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kutoa
elimu kwa jamii kutokana na athari zitokanazo na ukatili wa kijinsia.
Mashirika na taasisi hizo ambazo ni za
kiserikali na zisizo za kiserikali zinazopambana
kwa kiasi kikubwa kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapungua hapa
nchini ni pamoja na chama cha wahandishi wa habari wanawake Tanzania [TAMWA],
Mtandao wa jinsia Tanzania[TGNP], kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake[WILAC], Kituo cha sheria na haki za
binadamu[ LHRC] pamoja na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa
kijinsia hapa nchini.
Katika kupambana na changamoto mbalimbali
zitokanazo na ukatili wa kijisia serikali kupitia jeshi la polisi iliamua
kuanzisha kitengo cha madawati ya jinsia katika vituo vya polisi hii yote ni
katika juhudi ya kuhakikisha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapungua au
kukoma kabisa na kwa kiasi kikubwa madawati hayo ya mechangia kupunguza vitendo
vya ukatili wa kjinsia kwa kiasi flani katika jamii yetu.
Hivi karibuni chama cha wandishi wa habari
wanawake Tanzania TAMWA kilizindua
ripoti ya utafiti ya mwaka 2012/2013 ulifanyika katika wilaya ishirini za
Tanzania Bara na Zanzibar kuhusiana na hali ya ukatili wa kijinsia nchini,hali
iliyoonesha kuwa hali ya ukatili wa kijinsia bado ipo kwa kiasi kikubwa katika
jamii.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya utafiti kuna unyanyasaji mkubwa wa ukatili wa jinsia
hapa nchini kwani watoto wamekuwa wakibakwa, ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
na hata vipigo wanavyopata wanawake kutoka kwa waume zao ikiwa ni pamoja na
kutelekezwa kwa watoto na wanawake hapa nchini.
Hali hiyo uwafanya , watoto na wanawake wengi
kuathirika kisaikolojia na kutofikia malengo yao waliyokusudia kama vile
kuendelea kielimu kutokana na ndoa za utotoni hali inayo ongeza unyanyasaji
wawapo katika ndoa zao.
Kutokana na vitendo hivyo vya ukatili
kuendelea kuripotiwa kilasiku na vyombo
mbalimbali vya habari hapa nchini hivi karibuni nililazimika kumtamfuta
mkurugenzi mtendaji wa chama cha wanahabari wanawake Tanzania,tamwa bi Valerie
Msoka ili ni msikie anasemaje kuhusiana
na vipigo wavyopata wanawake kutoka kwa waume zao ambapo alisema kuwa vitendo
vya ukatili wa kijinsia vimeongezeka kwa wanawake kavile vipigo na vifo vinavyo
tokana na wivu wa mapenzi.
Amesema jamii inapaswa ielimike na kutambua
kwamba mapenzi sio kupigana bali mapenzi nikupendana hivyo amewashauri wanandoa
kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na sikwavipigo.
“Jamani mapenzi sio kupigana mimi naamini mtu
unaye mpenda huwezi kumpiga bali utamlinda kuhakikisha hapati madhara ” msoka
anasema.
Aidha msoka amewashauri wazazi na walezi
kuacha kuwa chagulia wachumba watoto wao,ikiwa ni pamoja na kuwaozesha watoto
wakiwa na umri mdogo na badala yake wawape elimu ya kutosha itakayowasaidia katika maisha yao na
kuwawawezesha kujitambua pindi watakapo olewa.
Amesma watoto wengi wanao olewa na umri mdogo
ndio wanao nyanyasika kwa kiasi kikubwa kwa sababu wengi wao hawatambui haki
zao, hivyo kunaumuhimu wakuwapatia watoto wakike elimu kwani pia itawawezesha
kujiinua kiuchumi na kuleta usawa wa kijinsia katika jamii na kupunguza dharau
na kuleta heshima kwenye ndoa zao hii itachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza
vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watototo wa kike nchini.
Pia ameitaka serikali kuangalia upya sheria ya
ndoa,sura ya 29 ya sheria za Tanzania pamoja na kwamba baadhi ya vifungu vya
sheria hiyo inaelezea juu ya haki ya mke kumiliki mali katika ndoa na masuala
ya mgawanyo wa mali endapo talaka itatolewa lakini baadhi ya vifungu vyake
nikandamizi hasa pale inaporuhusu
wasichana wadogo kuolewa wakiwa na umri wa miaka kuminanane na chini ya miamika
kumi nanane kwa ridhaa ya wazazi wake.
Amesema umri wa miaka kumi na nane ni umri wa kuwa shule sasa sheria zikiruhusu
umri huo msichana kuolewa inapelekea kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi
ya kupata elimu.
Hata hivyo ameongeza kuwa halikadhalika
kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi katika jamii kumeleta changamoto
kubwa kwa matumizi ya baadhi ya ya vifungu vya sheria hii hasa vile vinavyo
ruhusu ndoa za wasichana wadogo walio chini ya umri wa miaka 18, hivyo amewataka wajumbe wabunge maalumu
la katiba kuiyangalia kwa maakini sheria hii ili tunapopata katiba mpya sheria
hiyo kandamizi kwa wanawake iweimebadilika.
Watu wengi wamekuwa wakiishi katika ndoa hali
ya kuwa wanamanyanyaso makubwa huku wakivumulia kwa sababu mbalimbali pengine
kuepuka kuonekana wanaangaika kwa kuwa na huyu mara yule, au pengine mtu aliye
nae anakuwa ameshapata nae watoto hivyo hataki kuwasumbua watoto wake au
inawezekekana ugumu wa maisha pia unachangia kumfanya mwanamke avumulie kwa kuona
ana pakwenda.
Katika
kuhakikisha kuwa vitendo vya unyanyasaji vinapungua dhidi ya wanawake kituo cha msaada washeria
kwa wanawake WLAC kilizindua kitabu cha sheria ya ndoa na talaka jijini Dar Es
Salaam ilikumsaidia mwanamke kuijua sheria hiyo ili kumsaidia kutetea haki zake
awapo katika ndoa.
Kwamujibu wa kifungu cha 9(1) cha sheria ya
ndoa,sura ya 29 ya sheria za Tanzania,ndoa ni muungano wa hiari kati ya
mwanamke na mwanaume unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote hata hivyo
mambo ya msingi yanapaswa kuzingatiwa
ikiwemo hiari,kudumu,jinsi tofauti pamoja na umri ili muungano huo uweze
kukamilika kisheria.
Kwa mujibu wa sheria hii ya ndoa ni lazima
nilazima watu wanaotaka kufunga ndoa wawe wametimiza miaka 18 au
zaidi.Hatahivyo sheria hii inaruhusu mwanamke kuolewa akiwa chini ya umri wa
miaka 18.
Kifungu cha 17 kinaeleza kwamba mwanamke
ambaye hajatimiza miaka 18 anaweza kuolewa kwa idhini ya baba yake na kama baba
amefariki basi mama, na ikiwa wote wamefariki basi idhini hiyo inaweza tolewa na
mlezi wake.
Sehemu ya kitabu hicho kilichoandaliwa na
WLAC imesema kuruhusu wasichana kuolewa
chini ya umri wa miaka 18 kunamnyima fursa
ya kuendelea na elimu ikiwa ni
pamoja na kuwaweka katika mazingira magumu ya kuhimili majukumu ya ndoa, hivyo
kuhatarisha afya yao kwa kutokuwa na elimu ya uzazi.
Kwa kuzingatia mazingira ya sasa ya ukimwi
wasichana hawa wadogo wanakuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya
ukimwi kutokana na uelewa wao mdogo na pia kutokuwa na nafasi ya kutoa maamuzi juu ya miili yao.
Hivyo basi nivyema kwa wazazi na walezi
wakatoa kipaumbele elimu na sio ndoa japo wanadai kuwa ndoa ni heshima lakini
kwa mawazo yangu mimi naona ukimpatia elimu mtoto wa kike basi umemjengea
maisha yake na heshima katika jamii pia, wakati umefika sasa wakuachana na mila
potofu zinazo mkandamiza mwanamke na
kila mmoja kwa nafasi yake atumie uwezo aliyonao kwa kuelimisha na kumsaaidia
mwanamke pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha tunaondokana na mila kandamizi
kama ndoa za utotoni,ukeketaji na mauaji ya vikongwe hapa nchini.
Pia ni vyema ukiona mtu anafanyiwa vitendo vya
ukatili wakijinsia au wewe mwenyewe unafanyiwa vitendo hivyo basi usisite kutoa
taarifa sehemu husika ikiwemo polisi ili
hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwani kunabaadhi ushindwa kutoa taarifa
pale wanapofanyiwa vitendo vya kikatili kwa madai ya kuona aibu hali ianayo
rudisha nyuma mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili nchini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni