YESU NI JIBU

Jumatatu, 13 Oktoba 2014

KONGAMANO LA WWI NA MKUTANO WA INJILI LIMEFANA SANA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA WILAYANI TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM.

Kongamano ambalo limeandaliwa na chama cha Wanawake watumishi WWI jimbo la Temeke ambalo limefanyika katika viwanja vya sabasaba maarufu kama viwanja vya mwalimu Julias Kambarege Nyerere limefana sambamba na mkutano wa injili ambao umeendelea katika viwanja hivyo na maaskofu,wachungaji mbalimbali walihudhuria waumini wa madhehebu na dini tofauti pamoja na watu wenye mahitaji mbalimbali.
Konganano hilo na mkutano ulipambwa na waimbaji mbalimbali ambao walifika kumpa Mungu sifa na utukufu na watu wengi wamefunguliwa na kuponywa magonjwa na matatizo mbalimbali.
 Askoku mkuu wa jimbo la Temeke EAGT,mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania(CPCT) na ni mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT Mito ya Baraka Askofu Bruno Mwakibolwa.

 Askofu Mwakibolwa anakabithiwa zawadi na mkurugenzi wa WWI taifa EAGT kwenye mkutano wa Injili katika viwanja vya sabasaba


 Picha ya pamoja kati viongozi wa WWI taifa na jimbo la Temeke na baadhi ya viongozi wa jimbo hilo.
 Mchungaji wa kanisa la EAGT city Center mchungaji Florian Katunzi akifuatilia kwa makini mafundisho katika kongamano la wamama jimbo la temeke.

 Mchungaji Katunzi akipokea mkono wa pongezi na zawadi ambaye anakabidhiwa na mkurungezi wa WWI taifa akiwa na mkrugenzi WWI jimbo la Temeke mama Rachael Katunzi anayeshika zawadi.

  Viongozi wa WWI jimbo la temeke wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taifa WWI.

 Kutoka kulia ni mkurugezi wa WWI jimbo la Temeke mama Rachael Katunzi,wa pili ni mrs Paul Chisolo makamu mkurugenzi,wa tatu ni Mrs Kazoka ambaye ni katibu na wa nne ni mhasibu Carolin Kilango.



 


 Wanachama wa WWI jimbo la Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao wa jimbo hilo







Hapa sasa ni mwendo wa kupongezana kati ya wanachama wa WWI na viongozi wao katika viwanja vya Sabasaba wilayani Temeke Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa WWI jimbo la Temeke mama Rachael Katunzi akisisitiza jambo katika kongamano la wanawake

Makamu mkurugenzi mrs Paul Chisolo akiwasalimia wajumbe waliofika katika kongamano.
 Katibu Mrs Kazoka akisema jambo kwa wanachama wake ambao walihudhuria kongamano.
 Mhasibu Carolin Kilango hakuwa nyuma kuwasalimia wajumbe akiwa na makamu mkurugenzi.

 Askofu Mwakibolwa wa kwanza kulia kwenye mkutano wa injili sabasaba Temeke.









 Mchungaji wa kanisa la EAGT City Center akiwaombea wakina mama ambao walihudhuria kongamano la wanawake wa Injili jimbo la Temeke.
 Kundi la kusifu na kuzunguka uwanjali wakiwa na vibendera.
 Mwimbaji Jacob Mess Chengula akiwajibika katika  mkutano wa injili Temeke.


 Mwimbaji Solomo Mkubwa kutoka Nairobi Kenya akihudumu katika mkutano maarufu kwa wimbo wake utukufu apewe Mungu.

 Martha Mwaipaya Akiwa na mdogo wake Betris Mwaipaya wakiwajibika katika mkutano huko nyuma mchungaji akionekana akifuatilia kwa makini

 Kiukweli waimbaji walikuwa wengi sana hapa naye yupo Ibrahim Sanga na timu yake wakiwajibika.

 Mwimbaji kutoka Mbeya Emanuel Mgogo maarufu kwa wimbo wake msikilize Mungu akiwa na Bonny Mwaitege. 

 Bony mwaitege kulia na katikati ni Upendo Nkone na kushoto ni Rebeca Magaba.

Bony Mwaitege na vijana wake wakiwa jukwaani.




Mtangazaji wa WAPO Radio Sailas Mbise akiwajibika na timu yake ya kusifu na kuabudu kutoka kanisa la EAGT Mito ya Baraka wakimwabudu Mungu.


 Baadhi ya washiriki wa Kongamano na mkutano wakiserebuka.

Maoni 1 :

Unknown alisema ...

a well done report, this is what I call creative Journalism. Keep it Sne.

Chapisha Maoni