YESU NI JIBU

Jumapili, 12 Oktoba 2014

MWANACHUO AJARIBU KUJIONDOA DUNIANI KWA KUJIDUNGA KISU HUKO SINGIDA:

Ama kweli Adui anazidi kukimbizana na muda kwani tayari amafahamu kuwa muda wake ni mchache sana hivyo ameaua kutumia njia mbalimbali kuhakikisha kuwa anaingia katika ziwa la moto na waumini wengi.
Hata hivyo watumishi wa Mungu wanafundisha na kufanya maombi na maombezi kwa wale ambao wanakubali kumpokea Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.
 Ama kweli hapo ujione jinsi alivyojidunga. 
Katika mkoa wa Singida mwanachuo  ambaye anasoma katika chuo cha uhasibu TIA mkoani hapo aliamua kutaka kukatiza maisha yake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi hata hivyo amenusurika kufa baada ya jaribio la kutaka kujiua kwa kujikichoma kisu kushindikana
Kiukweli ukichunguza kwa makini utaona kuwa nyuma yake adui ameamua kutumia roho ya kujiua kwa lengo la kukatiza maisha ya binti Moza kwa sababu ya kumfumania mpenzi wake Je ? ni kweli kwamba mwanadamu anaweza kujidunga kisu ili kujiondoa duniani kwa sababu ya mpenzi na hata sio mume wala ni vyema kutafakari kwa makini maana adui yeye kazi yake ni kuangamiza na kuua yeye haoni uchungu wala hana huruma kwa mwanadamu.
 
Mwanachuo huyo  ambaye amefahamika kwa jina moja la  Moza ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza amefikia uamuzi huo  baada ya mwanachuo huyo kumfumania mpenzi wake wa kiume akiwa na mwanamke  mwingine.
picha kwa hisani ya Peruzibongo blog
TOA MAONI NA USHAURI WA KUWASAIDIA NA KUWAJENGA WANACHUO WASIWE KAMA HUYU,

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni