YESU NI JIBU

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

KUJIVUNIA AMANI NA RASLIMALI ZA TANZANZIA:


Nchi ya Tanzania imezungukwa na  Bara la Afrika na miongoni mwa nchi hizo za Afrika Tanzania ni nchi ambayo inajivunia vitu mbalimbali ikiwemo Vivutio mbalimbali ,na pia nchi yetu tunajivunia kuwa na kisiwa cha amani ulimwenguni kwa sehemu kubwa. 
Askofu Efrahim Mwansasu akiwa anatafakari jambo,
 Askofu Efrahim Mwansasu ambaye ni  Kiongozi wa huduma ya Hossana Life Mission amebatika kuzunguka bara la Afrika na hata katika nchi nyingine zilizopo nje mwa Afrika yapo mwengi amejionea na kungundua na kulinganisha na chini yangu ya Tanzania na kujivunia kuzaliwa nchini Tanzania

Nikwanini nimeguswa na swala nzima la amani ,nilikuwa nikisikia neno amani au nikilichukulia kama lilivyo utasema ni jambo ndogo sana na kulipuzia ila nilipokuwa katika masomo na vitabu mbalimbali na kuzunguka nchi nyingne nilijifunza na kugundua amani haipatikani kirahisi bali inatafutwa kwa garama kubwa  na ni lazima itunzwe na kulindwa kwa gharama kubwa.

Hivyo niwajibu wakila mmoja wetu kujifunza umuhimu amani na kugundua garama ya amani ,nakatika maisha yangu nilikuwa namuomba sana mungu anisaidie na anipe kibali kwa kuongozwa na roho mtakatifu malengo yangu niwe na kitu cha kipekee ambacho kitasaidia taifa langu usinipe kitu cha kibinafsi bali cha manufaa kwa taifa langu

Ndipo mungu akasema name kwa kupitia roho mtakatifu na kunipa kibali swala nzima la amani na kujua garama ya amani nikaona lisiwe kwa kuzungumza tu nitafute namna ambayo amani itakavyopaikana bila choyo wa upendeleo ndipo nikaja na waza la kuanzisha chuo ambacho kitakuwa na somo litakalo tujulisha  gharama ya amani.

Mbali  na kuwa na wito wa uchungaji pia ni mwimbaji na katika nyimbo zangu siachi kuzungumzia mtazamo wan chi yangu na mmwanzani mwa mwezi ujao nitazindua Albamu itakayobeba jina ndoto yangu .na tunarudi bale ukiwa na ndoto ukubali lazma ndoto yenye mafanikio ya kuimarisha taifa langu lazma itakuwa inawingwa na ili ufanikiwe lazma uwe na maadui uweze kufikia malengo flani na mimi Mwansasu napenda kuombea taifa langu na katika hizi nyakati tulizopo nchi yetu ipo katika hatari kubwa sana kuwekuwa na matabaka mbalimbali.

Unapoina nchi kunadalili kama hizo inabidi kugundua haraka akuwahi mapema kuzuia ile hatari tusijepotea na uwezi kumwachia mtu mmoj aongoze peke yake lazma apate msaadakutoka kwanachi anaowaongoza hivyo yapaswa kujua garama ya amani tusikurupuke kujibizana au kuchukulia jambo kazungmza flani na kuanza uchoshezi na kuyumbisha au kupotosha niwajibu wakukaa chini na kutafakari na kujua gharama na amani kwa hekima na busara na kurudisha watu kwa pamoja kwakuwa nchi yetu niya kisima cha amani.

Ukijaribu kuzunguka nchi za wenzetu na hata mataifa mbalimbali utalia na kusasa kwanini Tanzania wenzetu hawana amani kilasiku ni vilio kwa machafuko ya kwa kumwaga damu watu huwezi kukuta wapo katika mkusanyiko au kundi flani kwa kukaa pamoja na hata sehemu za kuabudia na kuwa na uhuru wa watu kuwakaribu na viongozi wao hata kukaa kwa pamoja  ,wenzetu kila kukicha wanahama wakimbilie wapi yote hayo yanatokea huenda wengine walipuuza  garama ya amani. Ombea taifa lako mtu wa mungu maana wakati unaruhusu.
Askofu Efrahim Mwansasu ambaye ni  Kiongozi wa huduma ya Hossana Life Mission akiongoza maombi kanisani kwake.
 waumini kanisani wakiabudu ndani ya kanisa kwa pamoja.


 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni