YESU NI JIBU

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

IFAHAMU BIBILIA YAKO KILA JUMAMOSI



1.Sadaka nini nini?
Jibu Ni aina ya uwekezaji katika ufalme wa MUNGU wenye kuleta faida  duniani na mbinguni.

2.Kuna aina ngazi za sadaka nazozifahamu zitaje?

Jibu:kuna aina nyingi za sadaka ila aina nne muhimu
a)     Zaka mwanzo 28:22b
b)     Malimbuko
c)     Dhahabu na
d)     Nadhiri

3.Ni sadaka ipi ni lazima kutoa na siyo hiari
Jibu ni zaka/fungu la kumi (Nehemia 13:12)

4.Tunda la Roho Mtakatifu limegawanyika katika mafungu matatu.
a)     Fungu la kwanza
·       Upendo  (warumi 5:5)
·       Furaha ; (wafilipi 4:4)na
·       Amani (warumi 5:1,waebrania 12:14)
b)     Fungu la pili
·       Uvumilivu;
·       Utu wema;na
·       Furaha. Wagatia 6:10
c)     Fungu la tatu
·       Uaminifu;
·       Upole; na
·       Kiasi. (Warumi 8:8,112:1-2)

5.Mfalme wa Babeli aliagiza mkuu wa matoashi  wake awateuwe vijana watakaosimama mbele ya jumba la mfalme walishwe na kutunzwa kwa muda wa miaka mitatu lakini walikuwepo baadhi ya wana wa  Yuda wataje hao wana wa yuda?

Jibu;Mkuu wa matoasshi aliwabadilishia majina
        I.            Daniael alimwita Belteshaza
      II.            Hanania =Shedraka
    III.            Mishaeli na;Meshaki
    IV.            Azaria =Abednego Daniel1:1-10

6.Yona alitumwa na MUNGU kwenda kuwahubiria watu wa ninawi kuacha njia zao mbaya na kutenda mema na kumtii Mungu bada ya kutenda uovu sana machoni pa MUNGU;baada ya Yona kufika katika nchi hiyo alizungumza maneno sita tuu ni maneno gani hayo na yanapatikana katika kitabu gani?

Jibu,Yona 3:4 Baada ya siku arobani Ninawi utaangamizwa.
7.Neno heshima lina maana gani?
a.       Answer Ni thamani ya utu ,utukufu,daraja la juu.
b.      staha ,adabu,nidhamu
c.       kitu anachopewa mtukama alama ya kuthaminiwa kwake.
8.Heshima ina sifa kuu mbili zitaje sifa hizo.
a.       sifa ya nje(thamani ya utu na utukufu)
b.      sifa ya ndani (inatokana na staha,adabu ambayo humsaidia mhusika kujulikana na kuwa maarufu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni