Unaweza
kuwa na maswali mengi ,mshangao zaidi kuwaza sana kuwa inakuwaje,na ni kitu
gani kinasababisha mchezaji kufa akiwa uwanjani ama akishangilia bao ambalo
amefunga au lilofungwa na mwenzake.
Hivi
karibu habari za kimichezo ambayo imetawala vyombo vya habari mbalimbali
duniani ya mchezaji wa soka nchini India Peter Biaksangzuala kufariki baada
kukimbizwa hospitalini kwa matibabu baasa ya kuanguka vibaya uwanjani
akishangilia bao lake.
Kiukweli
tunajifunza mengi kutokana na kifo cha mchezaji huyo kwani kuna mbinu za adui
ya kuangamiza maisha ya wanadamu hasa wale maarufu kwani ukibahatika kupata kitabu
kilichoandikwa na Emmanuel Agyarko kilichotafsiriwa na mchungaji Godwin Gunewe
ukurasa wa kumi na tatu utajua kinachoendelea.
Mnamo
mwaka 2003 kwa mujibu wa kitabu hicho mchezaji maarufu ambaye alijulikana kwa
jina la Marc-Vivian Foe kutoka nchi ya Cameroon alifariki dunia uwanjani akiwa
Ufaransa.
Kuna
baadhi ya watu maarufu kujiunga na imani nyingine ili kupata nguvu na uwezo wa
kuwa maarufu na wengine wanashindwa kutimiza masharti ambayo wamewekeana.
Ndugu
msomaji ni shauku ya mwandishi na msimamizi wa blog hii kuwa makini sana na
kusoma neno la Mungu(BIBLIA) ambayo ndiyo dira kamili katika maisha ya
kiroho,na pia kuwasihi wacheza mpira na mashabiki wao kutafakari kwa makini.
Jitahidi
kutafuta vitabu ambavyo vitakusaidia kujifunza yale yanayompendeza Mungu.
sasa endelea kupata kisa kilichotokea katika tibu Bethlehem
Vengthlang FC.
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.
Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa
mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kwa
timu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini
baadaye alifariki.
Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kupitia kwa mtandao wa Facebook,
ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha
mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka
na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia
alikuwa mchapa kazi.''
Toa maoni yako.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni