YESU NI JIBU

Jumatano, 2 Septemba 2015

TINDU LISSU AJITOKEZA NA KUJIBU BAADHI YA YALE AMBAYO DR SLAA AMESEMA NDIYO KILICHOSABABISHA AAJIUZULU SIASA ILA ATABAKI KUWATUMIKIA WANANCHI.

Dr Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Akihojiwa na redio station  redio Sauti ya Amerika VOA, Tundu amedai Dr Slaa ndio alihusika kufanya mpango wa kumkaribisha mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa CHADEMA na si vinginevyo. mh.Lissu anasema ameshangaa sana maneno aliyoyasema Dr Slaa  kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Anasema Dr.Slaa alikwisha kuteuliwa kuwa mgombea urais mwezi January na mwezi April akathibitishwa na kamati kuu,

Anaendelea kusema ameshangaa Dr.Slaa kusema Gwajima ndo alimleta Lowassa jambo ambalo siyo kweli kabisa, yeye Dr. Slaa mwezi wa tano ndo alianza kumtafuta Lowassa kwa kumtumia Gwajima

Anasema wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu, Dr.Slaa hakulala nyumbani aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.

Anasema dr. slaa asiwadanganye watanzania tatizo ni urais na mchumba wake.

Anasema ameacha siasa tangu siku ya kikao cha kamati kuu alipoandika barua ya kujiudhuru kwa nini amepokea mshahara wa mwezi huu?? kwanini anaendelea kutumia gari la chama la katibu mkuu na nyumba aliyonunuliwa na chama muulizeni awaambie kwanini anaendelea kunufaika na hayo yote toka CHADEMA???

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni