YESU NI JIBU

Ijumaa, 4 Septemba 2015

ASKOFU MUSTAAFU KUTOKA AFRIKA KUSINI, DESMOND TUTU, AMERUHUSIWA KUREJEA NYUMBANI KUTOKA HOSPITALINI, AMBAPO AMELAZWA KWA ZAIDI YA WIKI MBILI ZILIZOPITA.

Kwa mujibu wa wakfu wake, Tutu alikuwa akiugua maambukizi yaliyokuwa yamemkumba kwa mara kadhaa.
Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya nobel mwenye umri wa miaka 83, amekuwa na matatizo ya kiafya katika miezi ya hivi karibuni.
Hivi majuzi alilazwa hospitalini kutokana na maambukizi yaliyosababishwa na saratani ya tezi dume aliyokuwa akiugua.
Askofu tutu alistaafu rasmi mwaka wa 2011, lakini bado angali anasafiri kwa shughuli mbali mbali.
Taarifa iliyotolewa na wakfu wake ilisema kuwa Askofu huyo mstaafu amewashukuru wafanyakazi wa hospitali ya Cape Town kwa kumhudumia vyema.
Aidha alitoa shukrani kwa raia wa nchi hiyo kwa kumkumbuka kwa maombi yao na risala za heri njema.
chanzo BBC


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni