Mshauri mkuu wa kanisa la EAGT mchungaji Anyandile Mwakisyala.
Na Mwandishi Yonathan Landa
DODOMA.
Hatimaye kitendawili cha Nani kuvaa Viatu vya Askofu Moses Kulola kimeteguliwa leo na Mkutano Mkuu taifa uliotishwa kwa mujibu wa Katiba ya kanisa la Evangelistic Assemblies Of Tanzania hii leo.
Katika Mkutano huo uliokidhi vigezo vya kikatiba umechagua viongozi watakaongoza kanisa hilo kwa muda wa miaka mitano tangu sasa.
Mmoja wa wachungaji akihesabu kura
Nafasi ya Askofu mkuu
iliyokuwa inakaimiwa na Makamu wa Askofu wa Kanisa ndugu Asumwisye Mwaisabila
sasa nafasi hiyo amepata mrithi halali wa kupigiwa kura kwa mujibu wa Katiba
ambaye ni Mchungaji Brown Mwakipesile aliyeshinda kwa kura 1526 dhidi ya
Mchungaji John Mahene alipata kura 726.
Ikumbukwe kuwa
Mwakipesile kabla Nafasi hiyo alikuwa ndiye Katibu Mkuu wa Kanisa hilo kwa
kipindi kirefu sasa.
Nafasi ya Makamu wa
Askofu imeshikiliwa na Mchungaji John Mahene alipata kura 1490 dhidi ya
Mpinzani wake Leonard Mwizarubi aliyepata kura 563.
Aidha Nafasi ya Katibu
wa Kanisa hilo imechukuliwa na Leonard Mwizarubi kwa ushindi wa kura 1408 dhidi
ya Mchungaji Raphael Machimu aliyepata kura 416.
Vilevile nafasi ya
mtunza Hazina wa kanisa hilo imekwenda Kwa Mchungaji Pray-God Mgonja
ambaye ameshinda kwa kura 1011 na kumuangusha kwa mbali aliyekuwa anashikilia
nafasi hiyo Mchungaji Joshua Wawa kwa kupata kura 566.
Wakati huohuo Mkutano
Mkuu kwa pamoja walimpitisha Mshauri Mkuu wa Kanisa hilo ndugu Anyandwile
Mwakisyala pasipo kupingwa na mjumbe yeyote kwa kura ya ndiyo kuwa mshauri wao.
Uchaguzi huo
uliongozwa na Kamati Maalumu ya PCPT chini ya Mkuu wa kanisa la FPCT Taifa
Askofu Batenzi.
Picha ya pamoja kati ya viongozi wapya wa kanisa la EAGT na mshauri mkuu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni