Kampuni moja ya kutengeza madawa imelazimika kujitetea vikali
baada ya kupandisha gharama ya dawa ya Ukimwi kwa asilimia 5,000.
Hii
inamaanisha kuwa bei ya tembe moja ya dawa inayotumika kupunguza makali ya
ukimwi itapanda kutoka dola $13.50 hadi $750.
Kampuni
hiyo inayoitwa Turing Pharmaceuticals imelaumiwa na washika dau wa maswala ya
Ukimwi kwa kuongeza bei ya dawa hiyo ya Daraprim ambayo imekuwa mstari wa mbele
katika kuimarisha uwezo wa mwili wa mgonjwa aliyeathirika kupigana na
maambukizi mapya.
Turing
Pharmaceuticals ilinunua hati miliki ya dawa hiyo ya Daraprim mwezi uliopita
Agosti.
Mkurugenzi
mkuu wa kampuni hiyo Martin Shkreli amenukuliwa akisema kuwa faida
itakapatikana baada ya mauzo ya dawa hiyo itasaidia kugharamia utafiti wa dawa
mpya na zenye ubora zaidi.
Tembe
moja ya dawa hiyo ya Daraprim inagharimu dola moja pekee kutengeneza.
Hata hivyo bwana
Martin Shkreli anasema kuwa bei hiyo haijumuishi gharama ya kunadi dawa hiyo
wala usambazaji wake ilihali gharama imeimarika maradufu katika miaka ya hivi
punde.
''Katika
siku za hivi punde dawa za kupunguza makali ya saratani zinagharimu dola laki
moja (100,000) ilhali gharama yake asili inaweza kugharimu dola nusu milioni.
Daraprim
inauzwa kwa bei nafuu zaidi ikilinganishwa na dawa zinazotibu magonjwa sawa.
Shkreli
aliiambia runinga ya Bloomberg katika mahojiano ya kibinafsi.
Shkreli
alimsuta mwandishi mmoja wa habari kupitia mtandao wa Kijamii akimuita kuwa
''mjinga'' kwa kutaka kujua kwanini kampuni yake ilikuwa inaongeza maradufu bei
ya dawa hiyo muhimu katika vita dhidi ya Ukimwi haswa katika mataifa maskini
duniani.
Daktari Wendy
Armstrong kutoka muungano wa wauguzi nchini Marekani HIV Medicine Association
amekashifu sababu zilizotolewa kwaajili ya nyongeza hiyo kubwa ya bei ya dawa
hiyo.
Muaniaji
tikiti cha urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameonya kuwa serikali
yake itachukua hatua kali dhidi ya makampuni yanayofaidi kutokana na msiba wa
watu kwa kupandisha bei ya madawa maalum.
Source BBC.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni