Yametokea mapinduzi nchini Burkina Fasso, Afrika
Magharibi ambako jeshi limevunja serikali ya mpito ya nchi hiyo na kutwaa
madaraka.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi aliyezungumza kwenye runinga ya nchi hiyo,
Rais wa mpito Bwana MICHEL KAAFANDO amepokonywa madaraka bila kutoa maelezo
zaidi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Bwana KAFANDO na Waziri Mkuu wake Bwana ISAAC
ZIDA na baadhi ya mawaziri kukamatwa wakati kikao cha baraza la mawaziri na
wanajeshi watiifu wa wa zamani, Bwana BLAISE COMPAORE aliyejiuzulu mwaka jana
kufuatia maandamano dhidi yake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni