YESU NI JIBU

Alhamisi, 17 Septemba 2015

JIFUNZE NA KUFAHAMU AINA TATU ZA MABABA WA KIROHO DUNIANI.

 (1Wakoritho 4:15) Imeandikwa=Ijapokua mna waalimu kumi elfu katika Kristo walakini hamna MABABA wengi, Maana mimi (Paulo) ndio nilio wa zaa kwa Injili.
BABA WAKIROHO NI YUPI?
Baba wa kiroho,sio yule aliye kuongoza heti sala ya Toba,sio kweli,hilo hata washirika wangu wana wasaidia watu kuwaunganisha na Mungu,kwa kuwaongoza ukili wa kutubu dhambi,baada ya kuwashuhudia habari za Mwokozi Yesu.
Wakimaliza huwaleta kanisani,na Mimi ninawazaa kwa ile Injili yangu ya Ukombozi wa Roho,nafsi,na Mwili,na wanakua watoto wangu wa Kiroho,lakini sala ya Toba waliongozwa na mtenda kazi tu na sio mimi.
Hivyo BABA wa KIROHO ni yule ambaye injili yake uliielewa na kuipenda,na ukaamua kuomba au ukajikuta unamfuata wewe mwenyewe ili akuongoze,wewe unakua mtoto kwake,na yeye anakua BABA WA KIROHO,na tokea hapo anaanza kudili ma maisha yako,sio KIROHO tu hata kimwili na kukuchonga kitabia,kwa kukufundisha,kukuonya,kukuelekeza,kukukemea popote,maana umemkabidhi uskani akuongoze,nawewe una wajibu kusikia,kuelewa na kutii,kwa anaye kuongoza.
AINA 3 ZA MABABA KIROHO NI ZIPI?
(Luka 10:30-37) 
=Huyu ni mshirika aliyekua anasafiri safari,lakini njia moja na viongozi wa Kiroho au MABABA WA KIROHO,na tena kwa bahati zuri yeye mshirika alikua mbele katangulia.
Ghafla akatokewa na wahuni,wakampiga na kumjeruhi vibaya akawa amezimia nusu ya kufa,na kila alicho kua nacho kilipolwa na vibaka wale. Nakusudi la MAONO yake ya mwendo wa kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko ilikua,imekwamia pale.
MABABA 3 KATIKA NJIA MOJA.
Kwa Neena za Mungu,kabla hujatimiza kusudi la wewe kuepo hapa Duniani huwezi kufa,japo waweza kuteseka sana,katika kufikia kusudi lako.
(1) Ndipo akapita njia ile BABA wa kwanza,jina laki ni kuhani,au askofu leo akapita pembeni kabisa,ya huyu muumini aliye mahututi. Jamii ya Baba kama huyu,ndio wale ambao hukufurahia tu,ukiwa kanisani!! Unatoa zaka! Unaleta watu church!! Unaimba Praise!! Kama ni Bishop yeye huflahia tu wakati upo una chunga kituo cha kanisa lake,ukiwa na hatari za Mateso au ukifa!! Wanakuja church na kumfukuza mke wako na watoto, na pale church analetwa mchungaji wa kabila lake Bishop,tumeyaona hayo.
(2) Huyo Kuhani alipo pita pembeni ya mshirika,aliye mahututi, Ndipo tena akaja mlawi (Pastor) Naye ndio wale wale tu,wachungaji wa pesa (Mshahara)vikumi tu wakati ni mzima,huyu naye akalihepa tatizo la mshirika. Huyu namfananisha kama wale maaskofu,ambao ili uende kuombewa,ajabu na kweli unatozwa,kiasi flani cha pesa au kima,utazani unaenda kutazamiwa Ramri kwa mganga.
(3) Huyu wa tatu ndio BABA WA KIROHO WA KWELI, ambaye mimi na wewe tungependa kumfuata bila shaka yoyote.
Maana anatabia za kiungu kabisa,anaitwa BABA MSAMARIA YEYE ANATAMANI UWE NA MWENDO,KATIKA MAONO YAKO, hatamani kuona maono au makusudi yako yanafia njiani,kama anavyo amini my Senior Apostle Vincent Mkalla (Mdo 13:36)
KUMJUA BABA WA KWELI:
@ Akamwona akamuonea huruma.
@Alimfunga jeraha zake zote.
@Alikua na MAFUTA na divai akampaka.
@Akampandisha juu ya Punda wake.
@Akaenda kumpeleka kwenye nyumba ya wageni,akimhudumia kwa mali zake,au pesa tuseme,na sio kwa kunena kwa lugha mpya usiyo ijua,hapo ilikua moyo wa kulea na pesa ya Baba ndio inaongea.
@Bado tunasoma siku yapili,na zingine aliendelea kuja mpaka alipo kua amepona kabisaa.
@Biblia inatuonyesha alikua jirani naye, na tena Yesu anauliza katika hawa mababa wa kiroho 3 ni yupi aliyekua jirani yake? Wanaitika bila aibu ni Yule aliyo muonea Huruma,wakaambiwa nanyi fanyeni hivyo kama yule wa tatu.
PIGA PICTURE MABABA WENGI LEO WALIVYO.
@ Mtu mmoja aliwahi kuniambia,Apostle Bethania Simon mimi Baba yangu wa kiroho ni Nabii T.b Joshua,sababu zake sasa,heti siku moja alikua anamuangalia kwenye Tv akasema pokeeeaaaa basi alipo sema hivyo,huku anatunyoshea Mkono,mimi nikaanguka puuuuu chaliii,na toka siku hiyo akawa Baba yangu wa Kiroho. Mimi nikamwambia tu unapotea kwa kukosa ufahamu na akili nzuri za kiungu,maana hiyo siyo saini ya kua nibaba yako kiroho nk.
MABABA wengi leo wanaojiita,kua ni MABABA Hawana kabisa, moyo wa Kristo masiya.
Wengi hupenda kujipachika ubaba,wakati wao Bado ni watoto,ama Bado wana tabia za Kipagani,na utozi tozi tu,wakidhania huduma ni cheo,kama Meneja,au mhasibu.
Watu kadhaa wasio jitambua,na limbukeni wa kulewa heshima,za uanafunzi. Walikuja kuhubiri hapa church,na ikawa kawaida sana tu,cha ajabu na kweli ghafla unasikia mtu anatangaza Bethania ni Mwanangu wa Kiroho,Basi nacheeka tu kwakua yeye ndio kaongea ili apate sifa kupitia mimi kamanda wa vita, lakini nilijiuliza Ebo hivi!! Paka anaweza kumuongoza Simba? Au mjusi kafiri amuongoze,Mamba kweli? Teh tehe..Au mtu mwenye Roho wa Mungu aongozwe na mtu mwenye Roho mtakafedha?
DALILI ZA BABA ASIYEKUFAA KIROHO.
1.Ana Penda sana pesa na mali zako,kuliko kuku saidia usimame.
2.Anaye kuogopa kukushauri vizuri,ili usihame kanisa.
3.Anaye kutafutia tu madhaifu yako ili apate cha kuku hukumu.
4.Unapo muadithia usiri wako,yeye anakuhubiri madhabahuni j.p.
5.Ambaye mahubiri yake mengi,yamejaa kuitisha tu pesa,na kujisifu saana yeye.
6.Baba ambaye hakei kemei dhambi,kama vile Uzinifu nk Ogopa sana mtu anaye jilinda sana kwa mabaunsa,au kwa maneno yake,utasikia anahubiri,mimi mshirika anaye nisema vibaya atapata laana,na kufa ghafla,au nitayarudisha mapepo,na nagonjwa nilio yatoa, ukiona hivyo jua ndio wale waleeee.
7.Baba ambaye kwenye mapito yako,anajitenga nawewe,na anatoa tu visababu,oo lbd atakua amezini,au kanisema vibaya hivyo kapigwa huyu.
8.Mtumishi ambaye Mahubiri yake yamejaa,KUHUKUMU NA KUSHUSHA WATUMISHI WENGINE,NA KUWAZUSHIA UONGO,hapo kimbia  haraka.
9.Mtumishi anayeombea huku anakupapasa,maeneo Nyeti mwilini,hapo kimbia,maana kifuatachoni ni hatari .
10.Baba asiye tubisha watu,au kuhubiri wakovu na msamaha wa dhambi.
11.Pia jiepushe na Baba anayechukia na kuwa na uchungu,kwa watumishi wengine wanavyofanikiwa.Huyo ana Roho au mzimu wa umaskini,mkimbie haraka.
12.Baba anaye tumia sadaka au mbegu,kuhonga na kulala na makahaba,au hutumia kwa kulewa nk ukigungua kimbia huduma hiyo na umtafute baba wa kweli ambaye atakusaidia kuona mbingu,maana alivyo Baba ndiyo atakavyo kuwa mwanaye..ni mengi sana.
Unaweza kuwasiliana na Apostle Bethania kwa namba +255715 79 66 67. 
Unaweza kuwasiliana na blo hii kwa namba 0682672828.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni