YESU NI JIBU

Ijumaa, 4 Septemba 2015

KARANI KUFUNGWA JELA KWA KUKATAA KUTOA VYETI VYA NDOA KWA WATU WA JINSIA MOJA HUKO NCHINI MAREKANI.

Karani mmoja anayefanya kazi serikalini, amefungwa jela nchini Marekani kwa kukataa kutoa vyeti vya ndoa kwa watu wa jinsia moja.
Karani huyo, Kim Davis, anayefanya kazi kwenye jimbo la Kentucky, amesema hawezi kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana, kwani hilo linakwenda kinyume na imani yake ya Kikristo.
Jaji aliyesimamia kesi ya Kim Davis amesema mshtakiwa amekiuka sheria ya Marekani ambayo sasa inaruhusu watu wa jinsia moja katika majimbo yote kufunga ndoa.
Aidha, jaji huyo amewataka wasaidizi wa Davis waahidi kwamba watatoa leseni za kufungisha watu ndoa, hata kama ni wa jinsia moja.
Ikulu ya Marekani imeunga mkono uamuzi wa mahakama, ikisema hakuna mtu aliye juu ya sheria.
Sheria ya kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja ilipitishwa miezi miwili iliyopita. 

 chanzo ni DW.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni