YESU NI JIBU

Jumatano, 2 Septemba 2015

MAKAMU WA RAIS WA BARAZA LA MAASKOFU WA KATOLIKI TANZANIA (TEC) AMTAKA DR SLAA KUTOA USHAHIDI WA MADAI ALIYOYATOA JUU YA KUHONGWA KWA MAASKOFU WA KANISA HILO.

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amemtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi wa madai yake kuwa maaskofu wa kanisa hilo wamehongwa na Edward Lowassa. Akizungumza na MTANZANIA kwa simu yake ya mkononi, Askofu Niwemugizi alieleza kushangazwa na tuhuma hizo zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya maaskofu bila uthibitisho. “Hizo taarifa ndiyo nazisikia kwako, lakini kama kweli amesema hivyo kwa nini hakuweka ushahidi kuanzia majina ya maaskofu hao waliopewa fedha, kiasi na zilikopokelewa. Lakini kwa upande wangu binafsi sijapokea kiasi chochote kutoka kwa mtu yeyote. Askofu Niwemugizi alimtaka Dk. Slaa kutoa uthibitisho wa maaskofu wa kanisa hilo kupokea fedha kutoka kwa Lowassa waweze kutoa uamuzi. source: MTANZANIA

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni