YESU NI JIBU

Jumamosi, 20 Septemba 2014

WITO WATOLEWA KWA WATU WA DINI ZOTE KUHUDHURIA MAOMBI NA MAOMBEZI KATIKA VIWANJA VYA SIFA ZA YESU MANZESE JIJINI DAR ES SALAAM:



Imeelezwa kuwa ni vyema  watu kusimama na kumtumikia Mungu na kufuata taratibu na miongozo ya Kimungu ili waweze kuondokana na mateso ,taabu na shida mbalimbali zinazo wakumba katika maisha ya kila siku.
Wito huo umetolewa na mtumishi wa MUNGU mchungaji Paul Kaisi wa huduma ya Liko Tumaini Kwa Mungu ilipo katika Viwanja vya sifa za Yesu Manzese jijini DSM.
Ametoa wito huo wakati akifundisha neno la MUNGU na kusema watu wenye matatizo mbalimbali na kufungwa na dhambi kujitokeza kuhudhuria ibada hiyo kwa lengo la kufunguliwa na kuacha dhambi.
Aidha alisema kuwa watu wengi wamefungwa bila kujua na adui hivyo ni muhimu kuhudhuria ibada hiyo ya kufunguliwa siku ya jumapili hii kuanzia saa tatu kamili na kuendelea na maombi na maombezi yatafanyika kwa kila atakayehudhuria.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni