YESU NI JIBU

Jumatatu, 8 Septemba 2014

UKAHABA NI MBAYA SANA SASA JIONEE KAHABA MKONGWEUINGEREZA ANAYEDAI BADO ANA MVUTO

Bi Vogel-Couple kahaba mkongwe zaidi nchini Uingerez


Ama kweli dunia inakoelekea ni utata mtupu kwani mambo mengi yanaibuka ya aibu na mengina ya kushangaza,huku wengine wakishangilia na kufurahia kana kwamba ni mambo mazuri.
Hapa sasa fuatilia mwenyewe kwa umakini kikongwe ambaye ameamua kuweka bayana biashara yake ya ukahaba sasa je kwa muda wote alikuwa anafanya nini huku akijisifia kuwa yeye anaweza kazi yake hiyo kwa ufasaha,utashangaa kwa umri wake  ila kila mtu awe makini na kumtafuta MUNGU kwa bidii na juhudi.
Katika Umri wa miaka 85, Sheila Vogel-Coupe ni kahaba mkongwe zaidi nchini Uingereza na kwa umri huo bado anaweza kutengeneza Pauni 250 kwa saa moja kwa kazi yake.
Miaka minne baada ya kifo cha mume wake wa pili , Vogel-Coupe aliingia katika ukahaba ,kutokana na anachosema ni ukiwa anaosema ndio sababu ya kumfanya ajiingize kwenye biashara hiyo.
Akiwa na uwezo wa kuwaburudisha wateja angalu 10-kwa wiki , ameweza kukutana na wateja wengi kuliko unavyoweza kufikiria.
Akizungumza kuhusu wateja wake wa kiume, alisema : "kuna kitu wanachokiona kwangu. Ni hisia nzuri. Nafahamu nina mvuto sana."

 

 Bi Vogel -Couple anasema anaamini bado anamvuto.
 Akiwa amevalia sketi fupi (kimini) na viatu vyenye kisigino kirefu, Vogel-Coupe alijisifu na kujivunia kwamba bado anaweza kutengeneza pesa kutoka chumbani kwake.
Akielezea kwa nini ameamua kuifanya kazi hiyo, alisema: " Sababu ya muhimu zaidi ni kwamba napenda ngono. Hata kuifikiria tu inanifanya nijihisi vizuri''
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, Sheila atakuwa kwenye makala maalum yanayoangazia wanawake wakongwe makahaba 'My Granny the Escort'.
Onyesho hilo litaangazia pia wanawake watatu makahaba walio vikongwe zaidi nchini Uingereza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni