YESU NI JIBU

Jumanne, 16 Septemba 2014

JENGO LA GHOROFA TANO MALI YA KANISA LA SCOAN LAPOROMOKA.



Idadi ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni liliporomoka Jumamosi  wakati ujenzi ukiendelea.
Hadi kufikia siku ya  Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa,lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka.
Inaelezwa kwamba,mhubiri huyo wa kimataifa alipewa kibali cha kujenga ghorofa mbili,lakini mwenyewe akaamua kujenga ghorofa tano.
Uokoaji bado unaendelea na watu wengine mia moja na ishirini na nne walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia siku ya jumapili.
 Kiongozi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations(SCOAN) Nabii TB Joshua nyuma ni jengo liloporomoka

Baadhi ya majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.


 Waokoaji wakienddelea na shughuli za uokoaji.
 Picha hizi ni kwa idhini ya premiumt times -Micheal Abimboye,

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni