YESU NI JIBU

Ijumaa, 5 Septemba 2014

KULIOMBEA TAIFA NA VIONGOZI NI JUKUMU LA KILA MWAMINI BILA KUJALI ITIKADI ZA DINI,DHEHEBU,KABILA NA RANGI

Kongamano la maombi na maombezi juu ya taifa la Tanzania yamekuwa ya baraka sana mara baada ya mtumishi wa MUNGU mchungaji Florian Katunzi kuongozaa mamia ya watanzania wa dini na madhehebu mbalimbali kuliombea Taifa katika maombi ya kufunga na kuomba kwa siku tatu hivi karibuni.
Akihubiri katika kongamano la maombi na maombezzi ya kuliombea taifa alisema kuw ni lazima watanzania wasimame na kuachana na itiikadi za dini zao na madhehebu yao na kuungana pamoja na kusimama kama taifa mbele za MUNGU ili alikomboe nchi na watu wake.
Aidha alisema kuwa haijalishi kuwa taifa liweka katika misingi gani? ni lazima likombolewe na watu wake na kuwasihi watu wakliofika katika kongamano hilo la maombe na maombezi kukumbuka kuombea mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na uchaguzi ujao mwaka 2015,ili Mungu aingilie kati na kuleta amani naa utulivu.

 Mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT City Center mch.Florian Katunzi akiweka wakfu DVD ya mwimbaji ndani ya ukumbi wa PTA kabla ya maombi na maombezi juu ya Taifa kuanza.





 Hivi ndiyo ilivyokuwa ndani ya ukumbi wa PTA ambapo waumini mbalimbali wakiinua bendera ya Tanzania wakati wa kuliombea taifa.


 Hapa waumini wakiomba mbele za Mungu kwa pamoja wakiongozwa na mchungaji Katunzi ambaye hayupo pichani.

 Waumini wakifuatilia neno la MUNGU kwa makini ndani ya ukumbi wa PTA.


 Mwimbaji wa njimbo za injili Tumsifu Rutufu maarufu kama nabii Musa wa kizazi kipya akihudumu katika ukumbi wa PTA wakati wa kongamano la maombi.
Bwana Rutufu alishiriki kongamano hilo la maombi kwa siku zote tatu na amehudumu kwa siku zote na alisema kuwa ameshiriki katika konamano hilo ili kujijenga kiroho maana ni sehemu pekee ya kumwona MUNGU.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni