YESU NI JIBU

Jumapili, 14 Septemba 2014

IBADA KATIKA HUDUMA YA MAOMBI NA MAOMBEZI (BCIC)MBAGALA MAJI MATITU KANISANI MAJI MEUPE:

Askofu Michael Peter akifundisha neno.
Imeelezwa kuwa kuna maadui watatu wanaokwamisha maendeleo ya waamini ambao ni shetani ,mwanadamu na matatizo ,shida magonjwa ambazo zimewakwamisha watu wengi na kushindwa kumtumikia Mungu na kufikia malengo yao.
Akifundisha katika ibada ndani ya ukumbi wa BCIC iliyoko mbagala jijini Dar e salaam askofu Michael Peter Imani ameanza kwa kuelezea maana ya adui  kuwa kusema kuwa kwanza ni mtu anayemtendea mtu mwingine uovu au  hasimu
Pili ni jambo lolote linalodhuru au kuharibu mfano umaskini,magonjwa
Na tatu ni mshindani au mpinzani katika michezo
Aidha ameelezea Lengo la somo ni kuwapa namna ya  kufahamu jinsi na mbinu ya kupaambana na adui maana siku zote lengo la adui ni kuhakikisha kuwa unashindwa kufikia malengo na kuongeza kuwa wapo maadui katika maisha ya kila  ambao huwazuilia kushindwa malengo yako,maana kuna watu wanamaono makubwa na mazuri ambayo mtu akiyatekeleza anafikia malengo ila sasa kuna maadui wanaowazunguka na kuwakwaza kutofikia mafanikio.
Wakati mwingine watu wanapoteza furaha na amani na mamhusiano kwa ssababu ya tatizo la uadui na kwa watoto wa Mungu hakuna adui ambaye anaweza kukuzuilia mafanikio yako isipokuwa adui watakucheleweshea muujiza wako.
Hata hivyo wakati mwingine tatizo ulilonalo  halihusiani na Mungu maana wewe mlengwa umeshindwa kukaa chini ya uongozi wa Mungu mapaka unamruhusu adui kukwamishaa na kukuzuilia Baraka zako.
Huwezi kupambana na adui kwa kutumia silaha za kimwili kama bunduki,ngumi ama silaha yeyote ya kibinadamu lakini watu wengi wameshindwa katika vita vyao kwa kuamua kupambana na adui zao katika mwili.
Aliongeza kufundisha sababu za kufunga ambazo amezitaja kuwa ni kama ifuatavyo;
1.Kutafuta toba kwa Mungu (Isaya 58:8)
2.Kuanza huduma
Ili Mungu akupe ramani ya kuanzia na kile ambacho unataka kuanza
3.Kuweka wakfu matendo 14:23
4.Mahitaji mbalimbali
5.Mambo magumu mathayo 16:27
6.unapotaka upako au nguvu ya Mungu ingia kwenye kufunga na kuomba
Wakati wa kuhitimisha ameelezea aina nne za kufunga

a)    Mfungo mkavu
Esta 4:1-17 kufunga bila kula wala kunywa funga mwisho siku tatu ila Mungu anaweza kukuagiza ufunge Zaidi ya tatu lakini hakikisha kuwa ni Mungu
b)    mfungo wa kawaida   huu ni wa kunywa maji mathayo 4:1
kuanzia siku ya kwanza hadi arobaini
c)    mfungo nusu kuanzia saa 12 hadi 12 chakula ama maziwa Daniel 10 :23
Mfungo ni moja ya silaha zenye sana katika ulimwengu war oho ,dhidi ya shetani






Ni katika ibada ya kusifu na kuabudu ndani ya huduma ya BCIC mbagala maji meupe.

Mtangazaji wa wapo Radio Anasima Nathanieli akiwa kazini huko Mbagala Maji Meupe BCI wakati redio ikirusha matangazo moja kwa moja kutoka huko kanisanio kipindi cha makanisani Live.
mchungaji akifundisha neno la Mungu katka ibada ya masomo ya jumpili.

kutoka kulia nia askofu Michael Peter katikati mchungaji Peason Ndala na KUlia wakifuatilia neno la Mungu kwa makini wakati.

  Hapa ni watu ambao wamesalimissha maiasha yao kwa Yesu kama Bwana na MWokozi wa maisha yao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni