YESU NI JIBU

Alhamisi, 20 Agosti 2015

WACHUNGAJI WASAIDIZI PAMOJA NA WASHIRIKA WAELEZEA JINSI MCHUNGAJI WAO KUIONGOZI ALIVYOMALIZA SAFARI YAKE YA MWISHO DUNIANI,ASIFU NA KUOMBA SANA NA KUSEMA KISIMA KIMETIBUKA KILA MMOJA APOKEE MUUJIZA WAKE.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la COSAMA ambaye ni kifupi na maneno ya (kingereza come see man kutoka yohana 4:29) lilopo Maringo Kawe jijini Dar es salaam, mchungaji Edith Kabeya ambaye anajukulika sana kwa jina la mama kabeya amefariki akiwa katika huduma siku ya jumapili wakati wa huduma ya maombi na maombezi.
Akizungumza na gazeti la msemakweli mchungaji msaidizi Richard Mwangosi alisema kuwa mtumishi mama kabeya alikuwa akihudumia waumini katika ibada ya maombezi mara tu baada ya kipindi cha kusifu na kuabudu kuhitimishwa.
Mchungaji Mwangosi alisema kuwa mchungaji mama kabeya alisema kuwa kisima kimetibuka na kuwasihiu waumini wenye shida ,matatizo na mahitaji mbalimbali kujitokeza mbele madhabahuni ili Mungub awafungue maana Mungu ameshuka kuwahudumia watu wake.
Aidha aliongeza kuwa mara baada ya kuanza maombezi alimwaombea watu wawili na hapoa akaanza kuona kuwa anaishiwa nguvu na ndipo alipoamua kuelekea madhabahuni na kukaa na kuweka kipasa sauti pembeni na hapo ndipo wachungaji  na wahudumu walipoanza kumpa huduma ya kwanza na baadaye walimpeleka hospitalini na ndipo madktari wakadhibitisha kuwa tayari amepoteza maisha.
Mchungaji kufariki akiwa madhabahuni ni sawa na askari ambaye amefia vitani maana amlikuwa akifanya kazi ya Mungu mpaka mwisho wa maisha yake,maana hata mchungaji mama Kabeya alishawahi kutoka kauli kuwa yeye anataka Mungu amchukua akiwa mzima sio wakati akiwa mgonjwa,Alisema mchungaji Mwangosi.
Hata hivy alishwaambia kanisa zima kuwa waombe kwa bidii na juuhudi ili wakati wa kufa waweze kufa katika Bwana na wakati unapo mtumikia Mungu katika maisha yako.
Mchungaji Mwangosi aliwasihi washirika wa kanisa Hilo la COSAMA kushikamana na Kuendeleza kazi ya Mungu ambaye mchungaji mama Kabeya ameiacha ili kuwafikia wengi maana mchungaji yeye alishasema kuwa Mungu alishamwonesha siku ya kufa  ila hakuweza kumwambi mtu yeyote maana alisema kuwa watakuwa na hofu.
Kwa upande wa mtoto wake  mchungaji mama Kabeya ,Clopatra  John Kandoro alisema kuwa mama yake alifahamu siku yake ya kufa kwa maana kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita aliugua na akamuuliza Mungu kuwa je huu ni wakati wangu wa kufa,lakini jawabu alilopata ni kuwa sio wakati wake.
Aidha aliongenza kuwa kwa kipindi cha zaidi ya wiki kadhaa aliwaambia baadhi ya ndugu waliohudhuria kwenye sherehe ya kumwaga binti ya mwanaye aliwambia kuwa mimi naenda kupunmzika maana Mungu amenionesha ni pazuri sana ila sintaweeleza ila ni pazuri hivyo msiogope ila mshikamane na kuwa na umoja.
Clopatra aliongeza kuwa siku ya kuamkia jumapili mchungaji aliwaamsha wajukuu zake ambao alikuwa akiishi nao na kuwaombea sana,na kusema kuwa mama yake alikuwa akimtumikia Mungu wa kweli katika maisha yake.
Naye mchungaji Saimon Kamau kutoka Kenya ambaye amekuwa akishirikiana na mchungaji mama kabeya kwa muda mrefu,kwa maana huduma yake ilikuwa ikiwahudumia waumini wa dini mabalimbali katika huduma maombi na maombezi.
alisema pia kuwa kwa kipindi cha siku chache kuanzi ijumaa mchungaji mama Kabeya alikuwa katika hali ya kuwaaaga watu ambao walikuwa karibu naye na kuwasihi kuwa na mshikamano na kupendana kwa lengo la kumtumikia Mungu katika maisha yao ya kila siku.
Siku ya jumapili ambayo ni siku ambayo mtumishi wa Mungu alikufa alikuwa ni mtu wa furaha sana katika kipindi cha kusifu na kuchangamka na kuimba kwa futaha sana hukuwakiwasisitiza watu kumwimbia Mungu katika Roho na kweli.
Naye Juvenal Joseph Chami ambaye ni miongoni mwa watumishi wa karibu na mchungaji mama Kabeya alisema kuwa mtumishi hakuwa na tatizo lolote la kiafya maana yeye amefanya na mtumishi kazi kwa muda mrefu maana alimteua kuwa karibu naye katika kumtumikia Mungu.
Alisema kuwa katika kipindi cha kusifu uwepo wa Mungu ulikuwa mkubwa kwa viwango vya juu sana na alichofanya mtumishi ni kupokea kipaza sauti na kuanza kusema kwa sauti kuwa  kisima kimetibuka hivyo ni vyema kila mmoja kuja mbele mwenye mahitaji na matatizo mbalimbali maana Tayari Mungu ameshuka kuwafungua na kuwaponya.
Hata hivyo alianza kulegea na kuanza kuishiwa nguvu na kuelekea madhabahuni na kulala ambapo alipoteza maisha ndipo walipoamua kumpeleka hospitali kwa vipimo zaidi vya kitabibu maana walihofia kuwa inawezekana ni shinikizo ama kisukari alipanda lakini haikuwa hivyo.
Shemasi wa kanisa hilo ambaye anajukukana kwa jina la Zawadi Filipo Ngutu maarufu kama mama Toiro alisema kuwa siku ya jumapili mchungaji alikuwa amacheza sana kataika kipindi cha kusifu na kuabudu na alikuwa amevaa ngu nzuri kama ya bibi harusi na tena alikuwa akiomba kwa kupiga magoti kwa muda mrefu sana kwa kuelekea madhabahuni.
Aliongeza kuwa siku ya jumapili mtumishi alionekana mwenye furaha sana na kulikuwa na kijana mlevi ambaye alikuja kanisani siku ya jumamosi na siku ya jumapili alikuja tena ambapo baadhi ya wahudumu walitaka kumzuia maana alikuwa amelewa ila mchungaji aliwazuia na kusema kuwa mwacheni maana watu kama hawa Mungu anawapenda.
Mchungaji alicheza na kumsifu Mungu akiwa amemshikilia kijana huyo ambapo naye aliweza kufurahiya sifa pamoja na mtumishi wa Mungu na wakati sifa inaelekea ukingoni ndipo alipokea kipasa sauti na kusema kuwa kisima kimetibuka kisima kimetibuka kimbia mwenye shida na mwenye matatizo ili ufunguliwe na tayari Mungu ameshuka kuwaafungua waliofungwa,alisema Mama Tahiro.
Wakati akiomba alikuwa akisema kuwa Mungu awakumbuke wote ambao walihudhuria katika ibada hiyo ya jumapili maana ibada hiyo ilikuwa na nguvu sana.
Faransisca Justine au mama jemima ambaye ni mjuu kuu wa mama mchungaji Kabeya alisema kuwa bibi yake hakuwa na tatizo lolote la kiafya wakati akiingia kanisani.
alisema kuwa mchungaji aliomba yeye kwa muda wa nusu saa na akaanza kuwaombea waumini waliofika kanisani huku akisema kuwa kisima kimetibuka hivyo ni wakati wa kila mmoja kupokea kwa Mungu maana kisima kimetibuka.
Neno la mwisha ambalo mtumishi mama Kabeya alilisema kabla ya kufariki kwake kanisani li kuwa kisima kimetibuka hivyo ni wajibu wa kila mmoja kupkea kwa wakati wake maana tayari Mungu ameshuka kuwaponya na kuwainua watu wote wenye mahitaji mbalimbali

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni