Maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia walipelekwa katika eneo hilo ili kudhibiti umati huo kwa kuwa watu wanapiga foleni usiku kucha kuona muujiza huo wa alama.
''Tunaamini ni maono ya mtume wetu'', Aliou Traore ambaye anaishi katika eneo hilo aliiambia BBC.
''Watu
wamekuja kutoka Senegal kujionea huku baadhi ya mawaziri wa Mali pamoja na
viongozi wa dini wakitutembelea kuona muujiza huu'',alisema.
Bwana
Traore amesema kuwa alama hiyo imekuwa ikibadilika tangu ionekane mara ya
kwanza.''Mara nyengine alama hiyo inajifuta na kuonekana katika maeneo mengine
ya nyumba hizi.Baadaye inarudi'',alisema.
Mwandishi
wa BBC Alex Duval Smith mjini Bamako anasema kuwa watu hawalipi chochote kuona
alama hiyo lakini wanawacha fedha katika ndoo,ambazo familia ya Traore inasema
itazitoa kwa msikiti wa eneo hilo.
Wakati
ripota wetu alipotembelea eneo hilo,alama hiyo ilionekana kama kovu la simiti
la mwanamke aliyesimama.Picha za alama hiyo zimesambaa mjini Bamako kupitia
simu tangu ionekane siku ya jumamosi.
''Ni muujiza ,nimeuona'',alisema mwalimu wa shule ya msingi Aboubakar Diarra baada ya kuona ukuta huo.''Ni kweli.Ni alama kutoka kwa Mungu kwa Mali .taifa letu ni kubwa''.
Wafuasi wa Tijani ambao hupatikana magharibi mwa Afrika wanajulikana kwa kuheshimu miujiza.
Chanzo BBC
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni