YESU NI JIBU

Alhamisi, 27 Agosti 2015

ASKOFU MKUU WA WAPO MISSION INTERNATIONAL ASKOFU SYLVESTER GAMANYWA ATANGAZA MSIMAMO WAKE KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK.


Askofu Mwizarubi akiwa na askofu Gamanywa kwenye mkutano wa injili Arusha.
askofu Kazio waWAPO Mission Mbeya akiwa na askofu Gamanywa kwenye mkutano wa injili Mbeya
Kufuatia vuguvugu kubwa la kisiasa ambalo limeyakumba hata madhehebu ya dini, nimeamua kutangaza msimamo wangu kwa mambo ambayo nimeamua kuyapa kipaumbele ambayo ni haya yafuatayo:
1. Nitaendelea kuhubiri Injili ya ufalme wa Yesu Kristo ili kuendeleza kampeni ya usajili wa majina mapya kwenye kitabu cha uzima

2. Nitaombea na kuhamasisha amani na utulivu katika jamii hususan pale nitakapoona viashiria vya kuvunjika amani vinaingilia uhuru wangu wa kutoa huduma za kiinjili kwa walengwa
3. Kuanzia Mwezi wa Septemba nakwenda shambani kulima maharage, nyanya na matikiti na Mwezi wa Novemba nitakuwa navuna mazao yangu nikauze na kupata fedha za kuendesha huduma na maisha!
Natekeleza mithali isemayo: " ndugu wakigombana shika jembe ukalime; wakipatana chukua kapu ukavune"
Baada ya tarehe 25/10/2015 na 30/11/2015 tutawasiliana kwa ajili ya kufanya tathmini kuhusu matokeo ya nani kashinda na nani kashindwa!
Kwa hiyo kuanzia sasa mtu yeyote asinitaabishe na mambo ya siasa kabisaa!

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni