Mchungaji kiongozi wa kanisa la EAGT mlima wa Faraja lililopo yombo kisiwani Dar es salaam,mchungaji AIDAN MABUGA,amesema kuwa kanisa hilo ,limeandaa mikakati ya kupeleka injili vijijini.
Alisema
hayo siku ya jumapili wakati wa ibada ya kuhitimisha maombi ya mfungo wa siku
40, ambapo katika maombi hayo waliombea mambo mbalimbali ya kanisa pamoja na
uchaguzi mkuu wa raisi, wabunge na madiwani utakaofanyika octoba 25 mwaka huu.
Mchungaji
Mabuga alieleza kuwa amekuwa na mzigo wa kuhubiri injili tangu alipopata wito
wa kumtumikia Mungu miaka kadhaa iliyopita.
Aidha
akinukuu maandiko (matendo 20:24) alisema kuwa si vyema kuhubiri tu mjini wakati
kuna vijiji ambavyo wanauhitaji mkubwa wa neno la Mungu.
Tayari
Mch Mabuga ameshaanza kupeleka injili mijini na vijijini, mwaka juzi ambapo
alihubiri mkutano mkubwa katika mji wa Bujumbura nchini Burundi na mamia ya
watu walimpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao.
Hata
hivyo aliongeza kuwa mwaka jana alihubiri katika maeneo ya Bukoba vijijini na
Dar es salaam,na mwaka huu mwezi ujao atakuwa na ziara ya kupeleka injilimaeneo
ya vijiji vya Morogoro.
“Tuna
mshukuru Mungu ametujalia gari la kubeba waimbaji wachache na vyombo vya mziki,
pamoja na hayo bado tuna uhitaji mkubwa wa kupata gari kubwa la kubeba vyombo
vya kuhubiria pamoja na vyombo vikubwa vya injili ili kufika maeneo
mbalimbali.Tunakuwa tukishilikiana na madhehebu mbalimbali katika mwili wa
kristo.” alisema mchungaji Mabuga.
mchungaji AIDAN MABUGA
mchungaji AIDAN MABUGA akisisitiza jambo madhabahuni akiwa na mke wake madhabahuni.Mchungaji Mabuga akiongoza maombi ya kuhitimisha mfungo wa siku 40 katika kanisa la EAGT yombo Kisiwani.
Waimbaji wa kanisa la mlima wa Faraja Yombo Kisiwani kwa fundi umeme wakimsifu Mungu wakati wa kuhitimisha mfungo wa siku 40.
Baadhi ya watu wakishuhudia miujiza ambayo walitendewa na Mungu katika maisha yao.
Ni wakati wa maombi ya kuombea mipango mbalimbali ya kanisa pamoja na kuombea taifa la tanzania wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa octoba 2015 uwe wa amani na salama.
wakati wa maombezi ambapo mchungaji Mabuga akiwaombea waumini na wenye shida mbalimbali.
Baada ya mfungo sasa ni kusherehekea.
Aliwasihi wadau wa injili kushirkiana naye katika kuchangia ili kufikia malengo hayo kwa njia ya benki na kwa namba za simu.
Aliwasihi wadau wa injili kushirkiana naye katika kuchangia ili kufikia malengo hayo kwa njia ya benki na kwa namba za simu.
EQUIT BANK A/C NO: 3001211248922
JINA : EAGT MLIMA WA FARAJA.
TAWI LA QUALITY CENTRE
M-PESA : 0755 656749
TIGO- PESA : 0713 272368
Mawasiliano:- +255 755 656749
+255 713 272368
E- mail aidan.mabuga@yahoo.com
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni