YESU NI JIBU

Jumamosi, 8 Agosti 2015

MKUTANO UNAOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA UHASIBU MBEYA UMEENDELEA KULETA MABADILIKO KATJIKA MAISHA YA WAKAAZI WA MJI HUO AMBAO WAMEHUDHURIA NA KUFUNGULIWA KATIKA MATATIZO MBALIMBALI

Imeonekana kuwa Tanzania ni Nchi ya kwanza kwa kuamini masuala ya kishirikina na kufanya mambo ambayo hayampendezi Mungu.
Kauli hiyo imetolewa na askofu mkuu wa Wapo Mission International askofu Sylvester Gamanywa katika viwanja vya uhasibu Mbeya katika mkutano wa injili ambao umeandaliwa na huduma ya BCIC Mbeya.
Aidha amelisema kuwa  watanzania wanapaswa kuwa makini na kumtafuta Mungu wa kweli na kuachana na miungu ambayo inawapelekea kuwa wauwaji na hata kupelekea Taifa kuwa maskini wakati kuna raslimali nyingi ambazo zinaweza kufanikisha watanzania wote.   


Askofu Gamanywa akiwasili katika viwanja vya uhasibu jijini Mbeya na kusalimiana na askofu Kazio wa BCIC Mbeya
 Askofu Christopher Kazio kushoto akiwa na askofu Gamanywa kwenye viwanja va uhasibu wakifuatilia kwa makini waimbaji ambao wanahudumu katika mkutano wa injili.

kutoka kulia ni Alhappness Gamanywa akiwa Edina Malisa na nyuma anaonekana mshobozi.
Kutoka kushoto ni Bob akiwa na Linda ni washauri wa kiuchumi kutoka marekani wakifuatilia kwa makini mkutano wa injili uliohubiriwa na askofu Gamanywa katika viwanja vya uhasibu Mbeya.








 Amani mwasote akihudumu kwenye mkutano wa injili katika viwanja vya uhasibu jijini Mbeya.
Naye mwimbaji Happy Kamili mke wa mchungaji Antunus Kamili hakuwa nyuma katika uimbaji na pia yeye ndiye mshereheshaji katika mkutano huo(MC).

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni