YESU NI JIBU

Jumapili, 23 Februari 2014

VIONGOZI WA DINI NCHINI WAMETAKIWA KUONGEZA JUHUDI KATIKA KUHUBIRI YA AMANI KWA KILA MTANZANIA.


 Viongozi  wa  dini  na  madhehebu  yote   nchini  wameombwa  kuhakikisha  wanajitahidi    kuhubiri  amani  kwa  watanzania wote, ili  kulinda  amani  iliyopo  sasa  isipote, jambo  ambalo  litasaidia  matendo  kama  ya  ukatili  na  umasikini  kutokomezwa kama sio kwisha kabisa.

Hayo  yamesemwa  na  Mwasisi  na  mwanzilishi  wa  kituo  cha  nyumba  ya  maombi (HPC)  Apostle   Patrick  Kayimbi  Emmanuel  maarufu  kama  Apostle   P.K.E ,  alipokuwa  akihubiri    kwenye  kongamano  maalum   la  kuombea  amani  ya  Tanzania  linalofanyika  kituoni  hapo   Tabata- ugombolwa, ambapo  amesema  kuwa   watanzania  hawapaswi  kufunga  mikono  yao  juu  ya  maombi  ya  amani  na  badala  yake  amesema  wanapaswa    kuzidi  kumuomba  Mungu  kwani  mara  zote  shetani  hapendi  amani walionayo Watanzania ama wanadamu kwa ujumla.

“Sheteni  asitudanganye  kusema  tuna    amani, Hapana   shetani  anaandaa  vurugu  na  kutenganisha dini  moja  na  dini  nyingine,acha  nikwambie  hakuna  vita  kubwa  na mbaya  kama  vita  ya  dini  na  ukabila,vita  ya   dini  ikianza  tunaona  makanisa  kuchomwa  na  vita  ya kabila  pia  ikianza  tutaona  watu  wakitenganishwa  ndio  maana  Mungu  anataka  kanisa  pamoja  na  watanzania  wote  bila  kuangalia  itikadi  wala  dhehebu  kwa  pamoja  tuunganishwe  kwa  pamoja  tumwite  YESU  juu  ya  Tanzania” Alisema  Apostle  P.K.E  huku  akishangiliwa.washiriki wa kongamano hilo. 

Aidha  Apostle  P.K.E  aliwataka  watanzania  kutegemea  amani  ya  kutosha  nchini  kutokana  na   kongamano  hilo  kudhamiria   kuleta  amani    nchini,  huku  akiwasihi    wananchi  wote  kumrudia  Mungu  na  kumtafuta  kwaajili  ya  amani. Na  huku  akiwahakikishia watanzania   kuwa  ifikapo  jumatatu  ya  februari  24  Bunge  maalum   la  katiba  litakuwa  shwari   na  halitakuwa  na  misuguano  ya  wajumbe ,wabunge kama  ilivyokuwa  hapo  awali   siku  chache  zilizopita.
Pamoja  na  hayo  Apostle   P.K.E  alisema  kuwa   kongamano  hilo  pia  limelenga  kuombea  kampeni  mbalimbali  za  uchaguzi  zinazoendela ,pamoja   na  uchaguzi mkuu  utakofanyika  mwakani    nchini.
Hivyo,   kutokana  na   shughuli   aliwataka wanasiasa kutumia ndimi zao vyema wakati wa kuwepo kwa amaani maana ulimi  ni kiungo   kidogo ila madhara yake ni makubwa sana, kituo  cha  nyumba  ya  maombezi  imeona  ni  vizuri  kuombea  chaguzi mbalimbali  nchini.
Hali kadhalika   Apostle  P.K.E  alisema  kuwa   kituo  cha  nyumba  ya  maombezi  kipo  tayari  kuombea  wale  wote  wanaohitaji  uongozi  endapo  tu  wakikiri  kuacha  kwenda  kwa  waganga wa kienyeji.

“We  unayetaka  udiwani,  unayetaka  ubunge,  unayetaka  kuchaguliwa  tupo  tayari  kukuombea  ukisema  nitaacha  uganga  nataka  nikwambie  kwa  maombi   haya  tunayoenda  kufanya  uchawi  hautatumika  Tanzania  uganga wala  sadaka  ya  damu”Alisisitiza  Apostle  P.K.E   

Na  kwa  upande  wa  mhubiri  kutoka  nchini  Zambia  Apostle  Peter  Mwanga  alisema  kuwa  ni  vyema  kila  mtu    asimame  katika  nafasi  yake  na  kujiuliza ni  kitu  gani  amefanya  kwa   taifa  ambacho  kitafanya   watu  wamkumbuke.
Pamoja na hayo  ni  lazima  kila  mtu  awe  na  hofu  ya  Mungu   na    kujiulize  umefanya  nini  kwa  majirani  zako   na  maisha  yako   binafsi   na  kama  hujafanya  lolote , ndani  ya  nyumba  ya  bwana   lazima ufanye kitu ili  ukumbukwe  na  Mungu.       

Naye  diwani  wa  kata  ya  Segerea   Azuri  Mwambagi   aliyeshiriki pia  katika  kongamano   hilo  alisema   kuwa   miongoni  mwa  mambo  yanayopelekea  amani  kulegalega  ni  pamoja  na  suala  la  umasikini   na  kusema  kuwa  kwa  hali  ya  kawaida  ni  bora  mtu  achoke  mwili  kuliko  mtu   kukata  tama
 Hali  hiyo ni  hatari  sana  kwa  amani,Lakini  pia  bwana  Mwambagi  amepongeza  kituo  hicho  kwa  kuanda  kongamano  hilo  la  kuombea  amani  ya  nchi.


Itakumbukwa  kwamba  kongamano  hilo  lilianza  tangu  februari  16  na  linatarajiwa  kuhitimishwa  Machi   2 , huku  likijumuisha   jopo  la  watumishi  wa  Mungu  kutoka  takribani  nchi  tano  ambazo  ni  Namibia, Zambia, Canada, Dr  Congo,  pamoja  na  Kenya.

Maoni 2 :

Apostle P.K.E alisema ...

Mungu ibariki Tanzania

Apostle P.K.E alisema ...

Mungu ibariki Tanzania

Chapisha Maoni