YESU NI JIBU

Jumamosi, 8 Februari 2014

NI HUDUMA KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA PEFA MAZIZINI NI ZAIDI YA TAMASHA

Kazi ya kuhubiri neno la MUNGU huko Ukonga Mazizini  eneo la Uyakude imepamba moto pale ambapo waimbaji mbalimbali walifika na kuanza huduma ya uimbaji na kuungana na Nabii wa Neema askofu Elias Cheza ambaye yeye ana huduma huko Tabata. Akihubiri katika mkutano huo Askofu Chesa alisema kuwa ni hiari yako kumfuata YESU kama BWANA na mwokozi wa maisha yako ila ukikaidi na kukataa ni shauri yako wewe mwanadamu.

Hata hivyo watu wengi waliongozwa sala ya Toba katika viwanja vya kanisa hilo la PEFA linaloongozwa na kusimamiwa na mchungaji Jacob Elly.  
Hili ndilo kanisa la muda la PEFA Ukonga mazizini.

Hapa chini katikati mchungaji Jacob katikati na kushoto ni mke wake.

 Mch.Jacob akiteta jambo na mwimbaji wa Injili Bony Mwaitege.

Mch Elly akimwangalia kwa makini nabii wa Neema askofu Elias Chesa akimwelekeza kijana namna ya kutumia simu kwa kurekodi video wakati akihubiri katika viwanja vya kanisa ya PEFA Mazizini Ukonga. 
Mwinjilisti Dastan Mtoimzee wa injili ya sunami akihubiri huku mchungaji Elly mwenyeji akifuatilia kwa makini.
Nabii wa Neema Askofu Elias Chesa kulia akiwa na Mwinjilisti D.Mtoi.
Masanja mkandamizaji kushoto akiwa na Mwinjilisti D.Mtoi.
Waimbaji waliofika na kutoa huduma katika mkutano huo ni Emanuel Mgaya (Masanja mkandamizaji),Bony Mwaitege,Neema Jakonia,Tumaini Njole,Mc Joshua Makondeko,Neema Gaspa, Neema Jakonia na waimbaji wengine wengi,ni sawa na tamasha kwa jinsi waimbaji walivyojipanga kutoa huduma.  
Mwimbaji huyu ambaye anajiita Nabii Musa amekuwa kivutio kikubwa kwa watu wote waliohudhuria katika mkutano huo wakubwa kwa wadogo.



Neema Mwaipopo akihudumu na picha ya chini akiwa na Tumaini njole na Bony Mwaitege kwenye mkutano Ukonga Mazizini.


Hapa ni wakati wa Bony kuonesha jinsi anavyomtumikia MUNGU kwa njia ya uimbaji akiwa na vijana wake jukwaani.




Mtangazaji wa WAPO redio na pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili Silas Mbise akiwa na Masanja katika mkutano wa ukonga akishikiwa Mic na MC Joshua Makondeko.
Hapa Masanja akiwasalimia watu walifika kwenye mkutano na kuwatambulisha vijana aliongozana nao na kuanza kuimba wimbo wake maarufu NIKO BUSY NA YESU.



Mwenyewe chungulia stepu hizo za niko bize na YESU.

Neema Gaspa akihudumu na kundi la vijana wake wanoshirikiana nao katika kumtukuza MUNGU hapa ni katika mkutano wa Ukonga mazizini eneo la Uyakude.


Hao ni waimbaji ambao wamehudumu katika mkutano huo

Watu walivyofurika katika viwanja vya kanisa hilo la PEFA Ukonga Mazizini wakiinua mikono juu na kuweka juu ya vichwa vyao wakati wa maombi na maombezi.





Hakuna maoni :

Chapisha Maoni