YESU NI JIBU

Jumanne, 4 Februari 2014

MARA KWA YESU,OPARESHENI YA NENO LA MUNGU KUHUBIRIWA NA MAELFU WAFUNGULIWA.

Kila kona neno la MUNGU linahubiriwa kwa lengo la kuwafungua wengi walifungwa na nguvu za giza ,uchawi ,ushirikina na wale wote wenye matatizo mbalimbali wanfunguliwa na nguvu za BWANA YESU.Hata hivyo watu mbalimbali wamefika kumpokea bwana YESU kama Bwana na Mwokozin wa maisha yao ,hayo yote yamefanyika huko Musoma mkoani Mara ambapo kumekuwa na hali  mbaya kila kukicha vyombo vya habari vinaripoti mauaji yanayotendeka na kuendelea katika Mkoa huo.Watumishi wa MUNGU wakiongozwa na askofu wa jimbo la Mara askofu Godson Shaula
Makamu Askofu wa jimbo la Mara kaskazini la TAG askofu Godson Shaula akifuatilia neno la MUNGU kwa makini.

Daniels Mapunda Akitoa ushuhuda wake wake kabla hajaokoka katika mkutano wa Kange ambao unaendelea Musoma mjini maeneo ya machinjioni,anaongelea walivyokuwa wakiwafanya watu misukule,kuwapeleka na kuwatumikisha.
Alisema wachawi wanakuwa na dawa ya kumchukulia mtu ,wakichukua huwa wanakuwa na dawa wanayotumia kichawi kisha Yule anayetakiwa kuwa  msukule anatokwa na damu puani mdomoni na puani na kisha anaitwa na kuongozwa kwa kutumia kioo,hatimaye ndugu  hudhani kuwa amekufa Kumbe yupo nyumbani kafichwa sehemu,anasema mtu aliyechukuliwa msukule  Anatokwa na damu puani,lakini yote Tisa Mtu wa Mungu halogeki wala maiti yake haiwezi kuchukuliwa na wachawi alisema Daniel akihitimisha ushuhuda wake.
 Wachungaji wakifuatilia kwa makini ushuhuuda wa mchungaji Daniel kwa makini.
Wachungaji wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Musoma mjini wakisikiliza neno la MUNGU kwa makini.

Makamu askofu Godson wakiwa na mke wake.
 Umati wa watusi ukipita mbele kuombewa na kuokoka zaidi ya watu 67 wamemwamini Bwana YESU kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yao kwa muda wa siku tatu.






Mhubiri Daniel Mapunda kutoka Tanga katika kanisa la TAG Musoma  mjini maeneo ya machinjioni,akizungumza na waongofu wapya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni