YESU NI JIBU

Alhamisi, 6 Februari 2014

WAKAAZI WA UKONGA MAZIZINI KUFURIKA VIWANJA VYA KANISALA PEFA KUSIKILIZA NENO LA MUNGU.

Neema ya injili imehamia Ukonga -mazizini kwa kishindo ambapo mchungaji Jacob Elly amefungua kanisa jipya maeneo hayo ambalo linafahamika kwa jina la PEFA mara baada ya kuhama kutoka PEFA nyantira kwa lengo la kueneza neno la MUNGU kwa watu wote.
Akizungumza na blog hii mchungaji Jacob alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa watu wanampokea YESU kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao,na wale wanoonewa na kuteswa na nguvu za giza ,uchawi na ushirikina wanafunguliwa na BWANA YESU. 
Kwa hakika hapa tumefika kwa kishindo na kuhakikisha kuwa Bwana YESU anachukua sifa na utukufu maana yeye  pekee ndiye anaye stahili kupewa'.alisema mch.Jacob.


Naye mwinjilisti Dastani Mtoi wakati akihubiri katika viwanja vya kanisa hilo alisema kuwa hakuna nguvu nyingine yeyote inayoweza kushinda Nguvu za BWANA YESU.
Akielezea kwa undani alisema kuwa MUNGU pekee ndiye anayeweza kuleta mageuzi na mapinduzi katika maisha ya mtu binafsi,ukiamini kwa moyo wako na kukiri kwa kinywa chako utaokoka.
Mwinjilisti Dastani Mtoi akihubiri katika mkutano wa InjiliUkonga Mazizini eneo la Uyakude.

Watu waliofurika katika viwanja vya kanisa la PEFA kusikiliza neno la MUNGU.













Hakuna maoni :

Chapisha Maoni