Baada ya kupitia kwa ufupi falsafa ya kumilikisha kwa mujibu
wa Biblia, leo napenda kukujuza kuhusu mkakati ulioandaliwa na utekelezaji wa
kampeni ya OPERESHENI MILIKISHA. Mkakati huo ni kuundwa kwa Mtandao wa Vikundi
vya Maadili na Uchumi Tanzania (UVIMAUTA). Mtandao huu utaendeshwa kwa
kuzingatia sera iliyotungwa kwa madhumuni hayo, ndio nataka kukushirikisha
baadhi ya mambo muhimu yaliyomo katika sera hiyo:
Utangulizi
Suala zima la umikilishaji
halikuanzia hewani, bali ni mchakato ulioanza na mpango mkakati wa miaka 20 wa
MAADILI KWA KIZAZI KIPYA ambao
ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2010.
Mpango huu ulisheheni mikaakti mikuu mitatu ambayo ni 1. Ujersho wa maadili ya
kibibilia, 2. Unoaji wa vipaji vya uongozi wa kizazi kipya, na 3. Kumilikisha
uchumi endelevu kwa kizazi kipya.
Huu ukiwa ni mwaka wa 3 tangu
kuzinduliwa kwa mpango huu, mikakati miwili imefanyiwa kazi kikamilifu. Mkakati
wa Urejesho wa maadili ulifanyiwa kazi kupitia OPERESHENI TAKASIKA, Mkakati wa
uonaji vipaji vya uongozi umezalisha mchakato wa kuanzishwa kwa CHUO KIKUU CHA
UONGOZI WA KIMAADILI (MOLUT) na CHUO CHA VIPAJI(TIT) vyote vikisimamia na
wanataaluma waliobobea katika taaluma ya elimu.
Mwaka hu ndio tunashughulikia
kikamilifu mkakati wa tatu wa kumilisha uchumi ambapo tumeanzisha kampeni
maalum ya OPERESHENI MILIKISHA. Wakati huo huo tumepata wazo jipya (ufunuo
maalum) la kuunda mtandao wa vikundi vya maadili na uchumi Tanzania (UVIMAUTA)
ambao ndio utahusika kumilikisha uchumi kwa kizazi chenye maadili Tanzania.
Katika kutekeleza mkakati wa
kuunda mtandao huu, imetungwa sera maalum ambayo imezinduliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ikiwa ni
mwendelezo wa mpango mama aliouzindua mwaka 2010 wa MAADILI KWA KIZAZI KIPYA.
Katika makala ya leo tunaipitia sera kwa ufupi ili kupata picha kamili ya
mtandao wenyewe. Mambo tunayokwenda kuyapitia ni Maono, dhima na lengo kuu;;
kisha habari za haki na wajibu wa uanachama pamoja na maeelezo mengine muhimu.
Maono, dhima na lengo kuu
Maono ya Mtandao wa Vikundi vya
Maadili na Uchumi Tanzania (MVIMAUTA) ni;
“Kufikia mwaka 2028, vijana wa Tanzania wawe wanamiliki uchumi
endelevu ambao msingi wake ni ardhi
inayomilikiwa na watanzania wenyewe”.
Dhima kuu ni; “Kuhamasisha na
kuwawezesha vijana kumiliki uchumi kupitia vyanzo vikuu ambavyo ni; ardhi,
madini, mifugo, maji, na kilimo”.
Lengo kuu ni; “Kumkwamua kijana
kutoka katika hali ya umasikini hadi awe na makazi yake mwenyewe, ardhi kwa
ajili ya kilimo, na shughuli halali za kumuingizia kipato”.
Walengwa wakuu wakiwa ni makundi
ya: Vijana wanaohitimu katika vyuo vya kati na vyuo vikuu na wanashindwa
kupata ajira; Vijana waishio mijini kwa kufanya biashara ndogo ndogo zisizoweza kukidhi
mahitaji yao ; Vijana waishio vijijini wenye kutegemea kilimo cha jembe la mkono peke
yake; Vijana wajasiriamali walioanzisha miradi midogo ya biashara; Wanandoa
na wazazi/walezi kama wadau muhimu katika urithishaji
Haki na wajibu wa kila mwanachama
Kila mwanachama wa MVIMAUTA atakuwa na haki za msingi za kumwezesha
kutimiza matarajio yake ndani ya kikundi chake. Hata hivyo kupatikana kwa haki
kutazingatia jinsi anavyotimiza wajibu wake katika kikundi. Baadhi ya haki za
msingi za mwanachama ni: Kupewa taarifa zote zinazohusu maendeleo ya kikundi na mtandao mzima; Kushika
nafasi ya uongozi kupitia mfumo wa ukuaji wa mtandao; Kupata gawio stahiki la
faida itokanayo na uzalishaji wa miradi aliyochangia mtaji wake; Kupata mafunzo
ya kimaadili na kiuchumi; Kumilikishwa ardhi katika miradi itakayoanza baada ya
miradi ya mafunzo,na Kukopeshwa mitaji.
Kwa upande wa wajibu ni kwamba kila
mwanachama wa MVIMAUTA atatakiwa kutimiza wajibu wake katika kikundi chake.
Kutotimiza wajibu kwa mwanachama kutamfanya mwanachama huyo kutokuwa mwanachama
hai na hivyo kukosa haki zilizotajwa hapo juu.
Wajibu wa kila mwanachama, ndani
ya kikundi chake na katika mtandao kwa ujumla utakuwa ni kufuata misingi ya
dhana kuu ya MVIMAUTA na malengo yake makuu makuu saba (7) ambayo ni kama
yafuatayo: Kudumisha umoja wa kikundi na mtandao mzima; Kujenga uhusiano wa
karibu wa kufahamiana na kusaidiana; Kutoa michango ya kiibada na kimasaidiano;
Kushirikisha wengine maendeleo ya mtandao; Kushiriki mikutano ya kiibada ili
kuombeana na kujengana kiroho; Kujitoa kwa hali na mali katika shughuli za
uzalishaji mali na Kutumia vipawa na vipaji kwa manufaa ya mtandao
Umuhimu na upekee wa MVIMAUTA
Kiama ilivyo kawaida katika jamii,
kila j”ambo jipya” lazima lihojiwe kuhusu umuhimu na upekee wake, ndipo lipate
uhalali wa kuita “jambo jipya”! Kwa upande wa UVIMAUTA, nina hakika ni “jambo
jipya” kwa jamii ya kitanzania na huenda katika bara zima la Afrika kwa
kuzingatia sababu zifuatazo:
1. Muunganiko wa
maadili na uchumi.
Kwa karne nyingi kanisa la leo limetenganisha
”Maadili na uchumi” kama vitu visivyo na uhusiano. Hali hii imesababisha
udhaifu badala ya ufanisi. Kulingana na tafiti zilizokwisha kufanyika huko
nyumba, taarifa zake zinafanana katika kubainisha kwamba, ”uchumi bila maadili” huzalisha ufisadi
katika jamii. Na kwa jamii ya kitanzania hiki ndicho kinachosababisha
malalamiko na lawama dhidi ya wanaodaiwa kuitwa ”mafisadi”! Pili Maadili nayo bila uchumi ni kudumisha ufukara katika
jamii
Lakini kanisa la kwanza, la mitume wa
kwanza halikutenganisha maadili na uchumi! Utafiti wa kihistoria unaonesha
kwamba kanisa la jijini Yerusalemu lilidumu takribani miaka 40, likiwa na
maelfu ya waamini zaidi ya 30,000 lakini halikuwa na mtu mmoja maskini wa
kipato MVIMAUTA unarejea historia hii ukilenga kudhibiti ufisadi
na kuzalisha uadilifu; na kuhamasisha uchumi kwa kufuta ufukarana
na fikira tegemezi
2.
Fursa ya ukuzaji wa vipaji vya uongozi
Hivi leo
tunashuhudia kinyanganyiro cha kuwania nafasi za uongozi katika uutmishi wa
umma. Nafasi zenyewe ni chache, lakini baya zaidi ni kuwa jamii yetu haina ”kiwanda
maalum” cha kuzalisha viongizi wenye sifa na vipaji vya uongozi!
Kinachowasukuma walio wengine katika kuwania uongozi sio uwezo wa kuongoza bali
tamaa ya kujipatia kipato kupitia nafasi za uongozi au kaka ajira ya kawaida.
UVIMAUTA unakuja
na fursa pekee ya kukuza vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana watakaojiunga
na mtandao huu. Kumbuka kwamba, kila kikundii cha watu ishirini kitakuwa na
kiongozi wake. Na kila kikundi kizima
kinapoundwa kitapata mafunzo ya uchumi na uongozi.
Katika mafunzo ya
uongozi kila mwanakikundi anatafsiriwa kuwa ni ”kiongozi mtarajiwa” wa kikundi
kipya atakachokiunda yeye mwenyewe. Hivyo hivyo zoezi linaendelea la ”vikundi
kuzaa vikundi” ambapo mafunzo ya uongozi huendelea na fursa mpya za uongozi
kupatikana kwa kuundwa vikundi vipya.
Kigezo cha kuwa
kiongozi ni uwezo wa kuongoza na si vinginevyo. Uwezo wa kuongozi ni kipaji
maalum na ushahidi unathibitishwa pale ambapo kiongozi anazalisha viongozi
wengine wapya chini yake na hivyo yeye kupannda daraja la uongozi ili kusimamia
viongozi aliowazalisha mwenyewe!
3.
Fursa ya kukuza mitaji kupitia mtandao
Kikwazo kikubwa
ambacho kinadaiwa kuendeleza umaskini wa kipato katika jamii, ni ukosefu wa
mitaji. Kila mwenye wazo la kufanya mradi wa uzalishaji anajikuta anakabiliwa
na changamoto ya ukosefu wa mtaji. Wakati huo huo njia pekee iliyopo ya kupata
mtaji ni mikopo kuotka katika taasisi za fedha. Masharti kukopesha ni mkopaji
kuwa na dhamana ya nyumba au mali yenye thamani inayozidi kiwango cha mkopo
anaoutaka. Wengi hawana dhamana na hivyo kujikuta hawakopesheki.
MVUMAUTA unakuja
na jawabu la miaka mingi la ukosefu wa mitaji. Mfumo wa kuunda vikundi
unashughulikia changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa sababu, watu ishirini
wanaweza wenyewe kuchangiana mitaji kwa zamu kwa kila mmoja kupata mtaji mkubwa
wa mradi anaotaka kuufanya, na bila masharti ya kutoa dhamana.
Aidha, kikundi
kinapojiunga katika mtandao huu, tayari kinaskuwa kimeingia katika jamuiya
ambayo kuna vikundi vingine ambavyo vimeanzishwa kwa madhumuni ya uwezeshaji wa
vikundi visivyo na mitaji ili mradi vitaingia ubia ambao utahusisha kugawa
faida baada ya mauzo.
Huu ni uwezo wa
ndani ya vikundi na mtandao wenyewe. Isitoshe, kwa kupitia mtandao huu, kuna
fursa ya kuziendea taasisi za fedha na kuziomba mikopo kwa ajili ya miradi ya
mtandao na dhamana ikawa ni mtandao wenyewe kwa taratibu ambazo zi lazima
kuzielezea kwa hivi sasa. Ila wewe amini kwamba changamoto ya ukosefu ya mitaji
kwa wanachama wa mtandao inakuwa imeshughulikiwa kikamilifu!
Hapa fursa ni Mtandao wenyewe kuwa dhamana ya mikopo
ya vikundi badala ya wana vikundi kusumbuka kuweka dhamana ya mali zao binafsi.
4.
Fursa ya kuibua na kuendeleza vipaji
Kutokana na ripoti
ya maoni ya vijana wasomi wa vyuo vikuu ambayo ndiyo imechangia kuundwa kwa
mtandao huu; imebainika kwamba elimu inayotolewa na sekta yetu ya elimu, haina
mikakati ya kuibua na kukuza vipaji, bali imejaa nadharia tegemezi. Kwa mantki
hii mpaka sasa kuna upungufu wa fursa za kubaini vipaji mbali mbali na kuviendeleza
kwa kuviwezesha kimafunzo na mazoezi kwa viwango vya kimataifa
MVIMAUTA utatoa
fursa kupitia vikundi vyake kutoa mafunzo na fursa za mazoezi ambayo gharama
zake zitatokana na miradi maalum kwa madhumuni hayo. Isitoshe, kuna taasisi ya Bishop Gamanywa Foundation (BGF)
imeanzishwa kwa maono ya kufadhili mafunzo na mazoezi ya ukuzaji vipaji.
MVIMAUTA untanufakika na taasisi hii katika eneo hili lililotelekezwa!
Itaendelea
toleo lijalo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni