YESU NI JIBU

Jumamosi, 15 Februari 2014

MOTO UMEWAKA KATIKA NYUMBA YA MAOMBI TABATA UGOMBOLWA


Huyu ndiye mwasisi na kiongozi wa huduma ya nyumba ya maombi(HPE)Apostle PKE.


Huduma ya house of prayer center wameelezea kwa makini malengo ya kongamano la kuombea taifa na uchaguzi ili MUNGU alete amani na mshikamano bila kujali itikadi za dini,vyama vya siasa,ukabila na rangi ya mtu.
Akizungumza na waandishi wa habari mwasisi wa huduma hiyo iliyopo Tabata Ugombolwa jijini Dar es saalam Apostle Patrick Kayimbi Emanuel amlisema kuwa lengo ni kuombea amani iendelee kudumu katika Tanzania na hasa wakati huu wa bunge la katiba ambayo kwa sasa wanaenda kujadili suala la katiba mpya ili MUNGU aingilie kati na wawezekujadili yale yanayowalenga wananchi na sio dini wala chama cha mtu yeyote.
Aidha Apostle Emanuel amesema kuwa tarehe 22 Febr itakuwa siku maalum ya kukusanyika watu wote kwa pamoja kuombea taifa bila kuangalia itikali za dini wala dhehebu ili MUNGU ajifunue kwa wakati huu wa mchakato wa katiba mpya uende na kufanyika kwa amani,1Timotheo 2.1-2 na Yeremia 29:7.
"Mimi nawasihi wananchi wenzangu pamoja na viongozi wa dini mbalimbali kukubaliana na katiba ambayo tutaletewa hata kama wewe binafsi haikuwa maoni yako kwani hata huwa wakati wa uchaguzi raisi maranyingi hata kama hujamchagua ana kuwa raisi wa wote sio wa chama fulani anakuwa ni mkuu wa nchi husika,hivyo watanzania wote tuungane kuombea katiba iwe ya baraka kwa watanzania wote".alisema Apostle PKE.
 Hata hivyo aliongeza kuwa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wanasiasa wawe makini sana kwa kauli zao watakazo kuwa wanatoa iseje ikapandikiza chuki baina ya watanzania,sawa na waubiri au viongozi wa dini mbalimbali kuwa makini wakati wa kuhubiri asiwepo wa kuhubiri dini wala dhehebu la mtu mwingine bali wasimamie neno la MUNGU.
Wanasiasa hubirini sera zenu badala ya kupandikiza chuki juu ya chama fulani wakati wa kampeni kwani jamba kama hilo linaweza kutupeleka pabaya.
 Apostle PKE hakuwa nyuma kuelezea changamoto zinazomkabili katika kongamano hilo kuwa ni namna ya kuwapata viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali katika siku maalum ya kuombea taifa kwani malengo endelevu ni kuandaa kongamano la kila mwaka ambapo itakuwa rahisi kwa kila mtanzania kufika na kuombea taifa lake.
Pia hakuchelewa kumpongeza raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutoa fursa kwa kila mtanzania uhuru wa kuchangia maoni yake juu ya katiba mpya,hivyo 
ni vyema viongozi wa serikali kuhimiza viongozi wa dini na vyama vya siasa kuhubiri amani ya Tanzania isivunjike.Wahubiri watakaoshirikiana na Apostle PKE ni mchungaji Peter Mitimingi kutoka Tanzania,Bishop DrAbrahamMandrandelle kutoka Canada,Prophet Fodger Coetzee kutoka Namibia,Apostle Peter Mwanga kutoka Zambia,Ev.Freddy Kayimbi kutoka DR Congo na bishop Elie Kabengele kutoka Kenya.
Apostle PKE akizungumza na waandishi hawapo pichani.

Apostle PKE akiteta jambo na mwinjilisti Kaimbi
   Waandishi wakifanya mahojiano na mchungaji George Msigaro mmoja wa wachungaji wa huduma hiyo.
 Mke wa Apostle PKE Mariam akihojiwa na waandishi.

Maoni 1 :

Apostle P.K.E alisema ...

USIKOSE KONGAMANO HILO LA KIMATAIFA LA UKOMBOZI,MIUJIZA NA UNABII PAMOJA NA KUOMBEA NCHI YETU YA TANZANIA KUANZIA KESHO JPILI TAR.16FEB.HADI JPILI 2 MARCH 2014 .MA BUS YATAKUWEPO KUKULETA NA KUKURUDISHA BURE KABISA.
BUS KUTOKA KARIAKOO KUPITIA VINGUNGUTI HADI KANISANI
2.BUS KUTOKA GMBOTO KUPITIA KINYEREZI HADI KANISANI
3.BUS KUTOKA UBUNGO KUPITIA TABATA RELINI HADI KANISA.
JPILI BUS ITAONDOKA SAA1 ASUBUHI
JTATU HADI JMOSI BUS ITAONDOKA SAA7 MCHANA.
TSHIRT ,FLAG AND HANDKERCHIEF FOR THE BIG CONFERENCE IN HOUSE OF PRAYER CENTRE FROM 16TH FEB. TO 2ND MARCH 2014 ARE SELLING ALL OF IT FOR 10 US DOLLARS OR 15,000 TANZANIAN SHILLINGS

TSHIRT,KITAMBAA NA BENDERA YA KONGAMANO LETU LA KIMATAIFA INAUZWA KWA 15,000 HAPO HOUSE OF PRAYER CENTRE.KONGAMANO NI KUANZIA TAR.16 /FEB HADI TAR.2/MARCH/2014

TUPO TABATA UGOMBOLWA KITUO CHA SANENE MTAA WA KWANZA BAADA YA POLISI JAMII.
VYOMBO VYA HABARI WATAKUWEPO.IBADA YA JMOSI ITAKUWA LIVE UPENDO RADIO 107.7.
WAHI KESHO ASUBUHI
TAARIFU NA WENGINE.WOTE MNAKARIBISHWA

CONTACT +255766780580 / +255713075013
SHALOOM

Chapisha Maoni