YESU NI JIBU

Jumanne, 11 Februari 2014

ONYO KALI LATOLEWA KWA KUNDI LA WAKRISTO LA ANT-BALAKA.

Kama itahitajika kutumia nguvu ili kukomesha vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na kundi la anti-balaka, majeshi ya Ufaransa na yale ya Umoja wa Afrika yanapaswa kutumia sheria ya Umoja wa Mataifa ya kumaliza na kuangamiza kundi hilo.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean Yves Le Drian
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean Yves Le Drian
RFI

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amevitolea wito kikosi cha Ufaransa na kile cha Umoja wa Afrika kukomesha vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na kundi la wakristo la ant-balaka. "Kama itahitajika kutumia nguvu ili kukomesha vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na kundi la anti-balaka, majeshi ya Ufaransa na yale ya Umoja wa Afrika yanapaswa kutumia sheria ya Umoja wa Mataifa ya kumaliza kundi hilo", amesema waziri Le Drian.
 Jenerali wa Majeshi ya Ufaransa katika Operseheni Sangaris nchini jamhuri ya Afrika ya Kati Francisco Soriano amewatahadharisha waasi wa kikristo wa kundi la Anti Balaka jijini Bangui ambao wamekuwa kikwazo cha kupatikana kwa amani nchini humo kwa kuendeleza mauaji dhidi ya waislamu.“Wale wanaoidai kuwa ni wanamgambo wa kundi la wakristo la anti-balaka wafahamu kwamba ni maadui wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, hao ndio wamekua wakitishia usalama wa raia”, amesema jenerali Soriano wakati alipokutana na viongozi wakuu wa kidini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. 
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian ambaye anafanya ziara katika nchi kadhaa barani Afrika amezungumzia jana alipokua mjini Brazzaville, nchini Congo, juu ya mzozo wa jamhuri ya Afrika kati, amesema majeshi ya Ufaransa yataendelea kufanya kila jitihada kuhakikisha Amani inarejea nchini humo.
“Msimamo wa ufaransa nchini Bangui unaeleweka”, amesema LeDran, akibaini kwamba lengo la Ufaransa ni kufanya kila jitihada ili amani ya kudumu irejeye nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, “ hasa kuyapokonya silaha makundi yanayozimiliki bila kuegemea upande hata mmoja, huku serikali ya mpito ikiendelea na shughuli zake ili amani irejeye , na hali ya kibinadamu iweze kua sawa”, ameendelea kusema waziri huyo wa Ufaransa.
Le Drian alianza ziara hio ya kikazi tangu jumapili katika kanda ya Afrika ya Kati ili kuzungumzia jitihada za jeshi la Ufaransa kwa kurejesha hali ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Le Drian anatazamiwa kuendelea na ziara yake hadi mjini Bangui hapo kesho, baada ya mazungumzo leo na rais wa Congo, Denis Sassou Nguesso.
source RFI .

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni