YESU NI JIBU

Jumatano, 24 Oktoba 2012

KANISA LA KKKT KUFUNGA NA KUOMBA TAREHE 28 OCTOBA 2012 KUOMBEA AMANI TAIFA

Kufuatia matukio ya Uvunjifu wa Amani unaofanywa na kikundi cha watu wachache kwa mwamvuli wa "dini". Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limetoa waraka elekezi wa wachungaji Wake Wote Tanzania kuelekeza kuifanya siku ya tarehe 28 Oktoba, 2012 kuwa ya Kufunga na Kuomba kwa ajili ya amani nchini.

KKKT linakuwa kanisa la kwanza Tanzania kupitisha siku ya kikanisa la kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya nchi ilivyo Sasa.

Blog hii ambayo imefanikiwa kuutia machoni waraka huo uliotumwa na Maaskofu Dayosisi zote KKKT Wakuu wa Vituo vya Kazi za Umoja, KKKT na nakala yake kutumwa manaibu katibu wakuu, wasaidizi wa Maaskofu, Dayosisi zote KKKT, makatibu wakuu dayosisi zote kuwaelekeza kwamba tarehe 28 Oktoba ni siku ya kufunga na kuomba. 
Waraka huo umeelekeza "Kufuatia matukio ya kuchoma Makanisa yaliyotokea hivi karibuni,barua  inawataarifu kuwa siku ya Jumapili tarehe28 Oktoba 2012 imepangwa kuwa siku maalum ya kuombea amani katika nchi yetu. Pamoja na mambo mengine yaliyokwisha kupangwa kufanyika siku hiyo (28 Oktoba 2012)' tafadhali sharika, mitaa na vituo vya kazi za umoja vyote vya Kanisa letu vifanye maombi  hayo"

Kwa mujibu wa barua hiyo ya mtendaji mkuu wa KKKT, inawataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kuhimizwa kufunga na kuomba kwa kadri Roho wa Bwana atakavyowaongoza kuombea amani ya Tanzania. 
Blog ikinukuu sehemu ya mwisho ya barua hiyo inaeleza kuwa "Baada ya maombi ya siku hiyo, washarika wahimizwe kuendelea kufunga na kuomba kadiri Roho wa Mungu atakavyowaongoza"

Ipo haja na kanisa la Tanzania kuungana pamoja na Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania katika kuombea amani ya nchi.
SamSasali.Blogspot.com

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni